KIONGOZI wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava ameonyesha kuridhishwa na mradi wa ujenzi wa vibanda 34 vya biashara katika eneo la stendi kuu ya mabasi Halmashauri ya wilaya ya Liwale wenye Thamani ya shilingi milioni 137, 754, 450.00
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona utekelezaji wa mradi Mzava ameipongeza halmashauri hiyo kwa maono makubwa ya kuongeza chanzo kipya cha mapato kitakachowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo
Hata hivyo Mzava ametoa siku tatu kwa halmashauri hiyo kuandaa mikataba mipya watakayoingia na wafanyabiashara wanaotumia vibanda hivyo
" pamoja na kuwapongeza kwa kubuni chanzo cha mapato lakimi niwaagize halmashauri kuandaa mikataba mipya mutakayowapa wafanyabiashara hawa ambao wapo kwenye vibanda hivi ndani ya siku tatu kuanzia leo mei 25 hadi 29 mwenge wa uhuru uwe umeshapata taarifa ya utekelezaji wake" alisisitiza Mzava
Kwa upande wake kaimu afisa Mipango wa halmashauri hiyo Hamisi Abdallah amesema Ujenzi wa vibanda hivyo ulilenga kuongeza vyanzo vipya katika halmashauri hiyo ambapo hadi sasa halmashauri imeshakusanya shilingi milioni 25, 296,500.00 zilizotokana na ukodishaji wa vibanda hivyo kati ya bajeti ya shilingi 44, 480, 000.00 zilizopangwa kukusanywa kwa mwaka 2023/2024
" kukamilika kwa mradi huu, umewezesha mazingira mazuri ya wananchi kujiajiri wenyewe na pia kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kodi kwa TRA"
Kwa upande wake Johari Hamisi mfanyabiashara katika vibanda hivyo amesema toka halmashauri kujenga vibanda hivyo ha wao kukodishwa wamekuwa wakinufaika kutokana na kuwa na mazingira mazuri na ya kuvutia ya kufanyia biashara
No comments:
Post a Comment