MRISHO SOME Diwani wa Kata ya Fukayosi, akisalimiana na mmoja wa Madiwani baada ya kuapishwa rasmi kuwa diwani. Picha na Omary Mngindo.
...................................
Na Omary Mngindo, Bagamoyo.
DIWANI mpya wa Kata ya Fukayosi halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Mrisho Some ameanza kuwapigania wakazi wake, kwenye baraza lake la kwanza kuanza kutekeleza majukumu yake.
Some alianza kazi hiyo katika Baraza la robo ya tatu ambapo alianza kwa kuiomba TARURA wilaya hiyo kuiangalia barabara itokayo Kijiji cha Fitina haina Posho kuelekea shule ya sekondari ya fukayosi.
Akiwa katika kikao hicho Some alisema kwamba ndani ya Kata hiyo kuna changamoto kadhaa huku akianza na barabara kutokea Fitina haina Posho kuelekea shuleni huko.
"Mheshimiwa Mwenyekiti kwanza niwashukuru wanaFukayosi wenzangu, viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkuu wa Wilaya, Madiwani wenzangu na wataalamu wote kwa kunipokea," alisema Some.
Aliongeza kwamba "Katika Kata yangu ya Fukayosi kuna changamoto ya miundombinu ya barabara ya kuelekea shule ya Kata ya Fukayosi, ambapo barabara ni mbaya kupita maelezo, naiomba TARURA iiangalie barabara ile," alisema Some.
Katika baraza hilo diwani wa Viti Maalumu Ummy Matata Kisebengo alilalamikia kitendo cha kuhamishwa kwa wataalamu sekta ya afya, akielezea changamoto ya uchache wa watumishi huku akiomba halmashauri kuangalia adha hiyo.
"Mheshimiwa Mwenyekiti katika Hospitali yetu ya Wilaya tuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika sekta ya afya, kuna watumishi ambao walipelekwa kuongeza ujuzi nasikia wamehamishwa, hili Mwenyekiti tulifanyie kazi," alisema Ummy.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mohamed Usinga alisema kwamba changamoto hiyo wameipokea, huku akiahidi kuifisha ya Mkoa kwa taratibu zaidi
No comments:
Post a Comment