Na Hadija Omary, Lindi
Hatua ya Serikali kupitia wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) kuanza kujenga Mradi wa barabara ya Nyengedi-Mnara -Rondo yenye urefu wa km 1.15 kwa gharama ya Shilingi milioni 939,107,800.00 kwa kiwango cha lami kumeleta faraja kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Ujenzi wa Barabara hiyo umewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava mei 27, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa halmashauri ya Mtama na hivyo kupunguza gharama za matengenezo ya kila mwaka.
Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa (TARURA)Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema mradi unatekelezwa na Mkandarasi M/s.M.E & Company Limited ukiwa kwa sasa umefikia asilimia 15 ya utekelezaji na unakwenda kukamilisha urefu wa km 7.1 ambazo zinajengwa kwa sehemu tofauti zilizokuwa korofi zaidi.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 ukiwa katika halmashauri ya Mtama umekimbizwa kwa umbali wa Km 204.2 ukipita katika miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Bilion 2.526.
No comments:
Post a Comment