PAUL CHACHA AMKOSOA HECHE, ASEMA WASANII NA WANAHABARI WANAFANYA KAZI NZURI
Na Allan Kitwe, Tabora CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kufurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na wasanii na wanahabari nchini kwa kuwa wanaburudisha na kuhabarisha umma juu ya matukio mbalimbali kwa kuzingatia maadili ya kazi zao. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa Paul Matiko Chacha alipokuwa akihutubia umati wa wanaCCM, Viongozi na wakazi wa Mkoa wa Tabora waliojitokeza kumpokea jana Mjini hapa. Chacha amepinga vikali kauli iliyotolewa hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche akidai kuwa wanahabari wanaandika upumbavu na wasanii hawatendei haki wananchi. Amesisitiza kuwa wasanii, wanahabari na timu za mpira ikiwemo Simba na Yanga wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kwa maslahi yao pia, hawafanyi upumbavu kama anavyodai Makamu Mwenyekiti huyo wa CHADEMA. ‘Wanahabari hawaandiki upumbavu, wanatekeleza majukumu yao tena kwa weledi mkubwa na wasanii hawafanyi mambo ya kipumbavu, wanat...