Posts

TCRA KUSHIRIKIANA NA TBN KUSADIA KUZALISHA MAUDHUI YENYE TIJA

Image
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeahidi kufanyakazi na Mtandao wa Wana Blogu Tanzania (TBN), pamoja na vyama vingine vya waandishi wa habari ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe  19.Machi 2025 Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, alipokutana na ujumbe wa TBN ofisini kwake, katika kikao cha kujadiliana changamoto mbalimbali zinazowakabili Bloga nchini. “Sisi huwa tunapenda kufanya kazi na vyama ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao, badala ya kufanyakazi na mwaandishi mmoja mmoja…tunafurahi sana kufanyakazi na waandishi kupitia vyama vyao,” amesema Mhandisi Kisaka. Mhandisi Kisaka amesema kuwa TCRA imefurahi kukutana na TBN kwa kuwa wanafahamu kuwa Bloga wanasehemu kubwa sana kwenye maudhui ya ndani, na hata kwenye usajili wa TCRA Bloga wanachukua nafasi kubwa sana katika maudhui ya mtandaoni. “Kwa hiyo TBN mtakuwa silaha moja wapo nzuri sana ...

MFUMO WA USAJILI WAANDISHI WA HABARI KIDIJITALI UPO MBIONI KUKAMILIKA- MSIGWA

Image
  Na Mwandishi Wetu,  Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA) inaendelea na hatua za mwisho za ukamilishaji wa ujenzi wa mfumo wa Usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidigitali kwa Waandishi wa Habari nchi nzima - Journalists Accreditation & Registrations System (JARS). Mfumo huo unaotengenezwa na chini ya Idara ya Habari (Maelezo) na Wataalamu wa Mifumo wa e- GA, unalenga kurahisisha, kuongeza uwazi na kuimarisha utendaji kazi wa waandishi wa Habari kwa kuwapatia huduma ya usajili na utoaji wa vitambulisho vya kazi katika maeneo yao bila kulazimika kusafiri kwenda Dodoma au Dar es salaam kupata huduma hiyo. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari tarehe 16 Machi, 2025 katika Bandari Kavu ya Kwal...

WAZIRI KIKWETE KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI SONGWE.

Image
  Anatarajiwa kukagua na Kuzindua Miradi ya Maendeleo   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu -Mhe. Ridhiwani Kikwete Februari 23, 2025 amewasili mkoani Songwe kwa lengo la ziara ya  kukagua miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta  ya Elimu, Afya na Miundombinu   kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya wananchi . Mhe. Waziri Kikwete anatarajiwa kukagua na kuweka Mawe ya msingi katika miradi hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 700 katika Halmashauri zote za mkoa huo. Mara baada ya kuwasili katika  mkoa huo , Waziri Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Daniel Chongolo ambaye alimpa hali ya maendeleo ya Mkoa huo na maandalizi ambayo yameshafikiwa kwa ajili ya ziara hiyo. Vile vile Mhe.  Kikwete anatarajiwa pia kukagua Maendeleo ya Kituo cha Vijana cha Sasanda wilayani   Songwe ambapo atakagua  mradi wa Shamba la vijana lililopo kituo hicho.  Mhe Waziri Kikwete ame...

MRADI WA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU WATUA LINDI

Image
  NA HADIJA OMARY,  LINDI. Ili kufikia azma ya Serikali kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ya kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati kupikia wakala wa  umeme  vijijini (REA) imekuja na program ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya Leo January 3, 2025 alipokuwa akimtambulisha mtoa huduma hiyo Katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Amesema Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini ndani ya Mkoa huo Amesema Katika program hiyo kwa Mkoa huo wa Lindi Jumla ya Kaya 16,275 Katika Maeneo tofauti ya vijijini linatarajiwa kunufaika huku akibainisha  k...

NANI ATAKUWA MRITHI WA KINANA CCM?

Image
  Na Mwandishi Wetu. NANI atakuwa makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara? Ni swali ambalo limekuwa likiulizwa na makada wa CCM na hata wafuatiliaji wa karibu wa siasa nchini, hasa mwaka huu ambao Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu Rais, Wabunge na Madiwani. Jibu la swali hilo linatarajiwa kupatikana kupitia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliopangwa kufanyika mwezi huu, lakini kitendawili cha nani atakuwa Makamu Mwenyekiti atakitegua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Makamu mwenyekiti anayetakiwa kwa wakati huu ni yule ambaye atakuja kufanya kazi ya kuivusha salama CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anahitajika Makamu Mwenyekiti mwenye uwezo wa kukabili jukwaa na hadhira yake. Makamu Mwenyekiti asiye bubu wala mbabe, asiye mwenye ‘makando kando’, asiyekuwa mbinafsi, mchoyo na ambaye akisema atasikilizwa na kuaminiwa na wanachama na viongozi wenzake wa chama hicho tawala. Pamoja na majukumu mengine, makamu mwenyekiti atasimamia maadili ndani ya...

WANAFUNZI KIDOGOZERO WAISHUKURU LION.

Image
  Na Omary Mngindo, Kidogozero. WANAFUNZI wanaioishi katika mazingira hatarishi wakilelewa kwenye kituo cha Faraja, Kijiji cha Kidogozero Kata ya Vigwaza Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameishukuru Lion Club (Host) ya jijini Dar esa Salaam kwa kuwapatia misaada. Shukrani hizo zimetolewa na wanafunzi Enjo Frank na Faraji Ramadhani baada ya kupokea vifaa vya shule na vyakula vyenye shilingi milioni 1.6, vikikabidhiwa na Rais Mahmood Rajvan, Mountazir Barwani na viongozi wenzao walipofika kijijini hapo kuwafariji watoto hao 41. "Namshukuru Mwenyeezimungu kwani sikutegemea kupata msaada kama huu, utakaonisaidia katika masomo yangu wakati shule ikifunguliwa, mungu awasaidie na awaongezee pale mlipopunguza," alisema Enjo. Nae Ramadhani alieleza kwamba kwa msaada huo wa begi, madaftari  pamoja na peni vimempatia chachu ya kuendelea na masomo, huku akiahidi kufanya vizuri zaidi katika elimu yake ya Sekondari. Kwa upande wao wazazi Mohamed Ally aliishukuru Lion huku akiwahi...

WAZIRI KIKWETE AHUDHURIA MASHINDANO YA QUR ANI KWA WENYE ULEMAVU.

Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Ridhiwani Kikwete  ameshiriki mashindano ya Usomaji wa Quraan Takatifu kwa Wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Riziki Lulida yaliyofanyika jijini Dodoma. Katika mashindano hayo ambayo yalikutanisha Wenye Ulemavu kutoka makundi mbalimbali, Waziri Kikwete alitoa  salamu za serikali na kuwakumbusha kazi nzuri anayoifanya Mh. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri Ya Muungano ya Tanzania ikiwemo Mkakati wa kusimamia Haki na Ustawi wa Wenye Ualbino, Sera ya Usimamizi wa Teknolojia saidizi na mapitizo ya sera mbalimbali zinazosimamia maslahi ya Wenye Ulemavu ikiwemo sera ambazo haziendani na mazingira ya sasa.  Aidha alisema Wizara kwa upande wao walieleza walipofikia katika kila maelekezo ya Mh. Rais, Ilani ya uchaguzi na miongozo mingi imetolewa.  Wameendelea kumpongeza Muandaaji wa mashindano hayo Bi. Riziki Lulida, na taasisi yake na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWAT...