Posts

NAIBU QADHI MKUU AMPONGEZA SHIRAZI KWA KUJENGA MSIKITI DAR ES SALAAM.

Image
  Na Mwandishi Wetu Naibu Qadhi Mkuu, Ali Khamis Ali amempongeza mfanyabiashara Shiraz Rashid kwa kujitolea kujenga Msikiti wa Imam Ali Bin Abu Talib eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam. Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Msikiti huo hafla ambayo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali mbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao. Alisema lengo la kujenga Msikiti huo ni kuhudumia waumini kwenye ibada ya swala tano na aliwashauri watanzania wengine kuiga mfano huo kwani hiyo ni kazi ya MwenyeziMungu. “Tunatoa wito watu wengine waige mfano wa Shiraz ili tujenge nyumba za ibada kwani nyumba hizi zinasaidia kurejesha utulivu na amani kwa watu kufanya ibada, huu ni moyo wa upendo wa ndugu yetu aliouonyesha kwa hiyo natoa wito kwa wengine waige,” alisema Naye Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh, Walid Kawambwa, alisema ujenzi wa Msikiti huo ni jambo jema na kuwataka watu wengine kuanzisha ujenzi kama huo kwani hiyo ni kazi ya MwenyeziMungu. “Mtume al...

WATOTO 1,500 WENYE MATATIZO YA MOYO WASUBIRI MSAADA.

Image
  Kikwete kuongoza harambee matibabu yao mwezi ujao Na Mwandishi Wetu RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuongoza harambee ya kuchangia matibabu ya watoto 1,500 wanaougua magonjwa mbalimbali ya moyo ili wapate matibabu kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Naibu Spika wa Bunge, Musa Azzan Zungu, wakati akizungumzia harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika tarehe 2, Novemba mwaka huu kwenye hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam. Alisema takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kati ya watoto 100 wanaozaliwa, wawili wanakuwa na matatizo ya moyo na kwamba hadi sasa watoto 1,500 wameandikishwa kwaajili ya kupata matibabu hayo lakini hawana uwezo. Naibu Spika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Heart Team Africa Foundation, alisema watoto hao wasipopata matibabu hayo kwa wakati wanaweza kupoteza maisha hivyo aliwaomba watanzania kujitokeza wakati wa harambee hiyo kuwachangia matibabu. “Nawaomba wat...

MACHIFU WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUENZI UTAMADUNI.

Image
  Wasema atasaidia kurejesha maadili yanayoendelea kuporomoka Na Mwandishi Wetu VIONGOZI wa Kimila kutoka mikoa mbalimbali nchini, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Tamasha la Utamaduni la Kitaifa pamoja na kuongeza thamani ya viongozi wa mila iliyoonekana kushuka kwa miaka mingi. Wamesema hatua hiyo ya kuthamini, kufufua misingi na kuenzi tamaduni zilizokuwa zimeanza kuwekwa kando itasaidia kwa kiwango kikubwa kulinda maadili na tamaduni za Kitanzania. Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani Ruvuma linakofanyika kongamano hilo la tatu la utamaduni la kitaifa, viongozi hao wa kimila wamesema kwa miaka mingi mila na tamaduni za Kitanzania zilionekana kutokuthaminiwa lakini Rais Samia ametambua umuhimu wake na kufufua. “Tunamshukuru Chifu Hangaya (Rais Samia), yeye kama kiongozi namba moja wa Machifu wote Tanzania, ameona umuhimu wa kuenzi mila na tamaduni zetu ambazo zilikuwa zimeachwa kupewa kipaumbele sana, kwa kifupi ni kwamba amezifufua na kuupa thamani kubwa u...

TASSIM YAANDAA MAONYESHO YA VIWANDA VIDOGO DODOMA.

Image
  Na  Mwandishi Wetu SERIKALI imewaalika wananchi na wadau mbalimbali kuhudhuria mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Sera mpya ya biashara ndogo ndogo (SMEs) utakaofanyika mkoani Dodoma . Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. John  Simbachawene, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya viwanda vidogo vidogo (TAMISID). Siku ya viwanda vidogo vidogo inayotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu mkoani Dodoma inaratibiwa na Chama cha Wenye Viwanda Vidogo Tanzania Association of Small Scale Industries and Manufacturers (TASSIM). Alisema serikali ilikusanya maoni ya watu mbalimbali kwenye awamu ya kwanza hivyo imeamua kuandaa mkutano wa awamu ya pili kuchukua maoni kwa wale ambao walikosa nafasi kwenye awamu ya kwanza. Alisema mkutano huo utafanyika wiki hii mkoani Dodoma na kuwataka wananchi,  wajasiriamali, wafanyabiashara kushiriki kwenye mkutano huo ili watoe maoni ya kuchangia kuboresha sera hiyo. “Wizara inaendelea...

RAIS SAMIA AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI IGP WAMBURA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024

TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA LAFUNGULIWA SONGEA.

Image
Na Mwandishi Wetu, RUVUMA WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amewaasa watanzania kuzingatia miiko, mila na desturi za kitanzania na kuwarithisha watoto na vijana ili kujiepusha na tamaduni za kigeni zisizofaa kwa jamii. Aidha, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwachukulia hatua kali wale wanaoua mila na desturi za watanzania kwenye mitandao ya kijamii. Akizindua Tamasha la tatu la Utamaduni Kitaifa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea, alisema kusipokuwa na utamaduni hakutakuwa na utu na wasipouenzi hawatauendeleza. “Ili Taifa liwe hai lazima tuenzi na kuendeleza utamaduni wetu, na lazima turithishe utamaduni wetu kwa vijana na watoto na lazima tuwafundishe watoto wetu mila na desturi za kitanzania, Kiswahili tuwafundishe miiko mbalimbali na historia yetu kwa kuwa hawa watoto ni taifa la kesho,”alisema. Alisema katika maadhimisho ya tamasha hilo ilitolewa semina ya maadili na utamaduni iliyofundisha jinsi ya kuenzi utamaduni na namna ya kukabilia...

MADAKTARI BINGWA WA MAMA SAMIA WAWEKA KAMBI MKOANI LINDI

Image
  Na Hadija Omary, LINDI. Wananchi Mkoani Lindi wametakiwa kutumia siku sita za ujio wa madaktari bingwa na ubingwa bobezi wa Rais Samia kupata huduma za kibingwa kwa karibu katika hospitali za Wilaya  za Mkoa huo   Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt Kheri Kagya Jana  septemba 16, 2024 wakati wa kuwapokea madaktari hao bingwa na bingwa bobezi wa Rais Samia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa lindi kisha kuwakabidhi kwa waganga wakuu wa halmashauri sita za mkoa huo Madaktari hao watakuwepo kwa muda wa siku 6 kuanzia Jana Septemba 16 hadi 21 wakitoa huduma za kibingwa kwenye hospitalli zote za halmashauri Mkoani Lindi lengo likiwa  kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa bobezi karibu zaidi na wananchi pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wa afya kwa ngazi ya halmashauri kutoa huduma hizo za kibingwa. Dkt. Kagya ametaja madaktari waliopokelewa ni pamoja na madaktari bingwa wa huduma za magonjwa ya kike na uzazi, upasuaji, mfumo wa mkojo, magonjw...