Posts

Manispaa Ya Ubungo Yapitisha Bajeti Ya Billioni 84, Mwaka Wa Fedha 2019/2020

Image
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yapitisha Makadirio ya beti ya 2019/2020 Kutumia Kiasi cha Tsh Billioni 84.6 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.  Akisoma Hotuba yake Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo,Mh Boniface Jacob, amefanunua kuwa katika pesa hizo serikali itatoa ruzuku ya Billioni 65.5,Millioni 750 ni  michango ya Wananchi na billioni 18.4 ni Makusanyo ya ndani. Ambapo katika matumizi yake fedha hizo,Billioni 72.3 ni Mishahara ya watumishi,Na kiasi cha billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi Mbalimbali ya Maendeleo Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha billioni 8.3 sawa na Asilimia 60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya Miradi ya maendeleo Mstahiki meya ametaja Vipaumbele 11 vya Halmashauri vilivyomo katika Bajeti hiyo kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza pesa za kujengea Makao makuu ya Halmashauri kiasi cha Millioni 700, Kuanza kujenga Hospitali ya wilaya kwa kiasi cha Tsh Millioni 250 Kuten...

AFISA ANAYETUMIA CHEO KUOMBA RUSHWA YA NGONO AUMBUKA.

Image
AFISA Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Valintine Mbai ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Halmashauri hiyo ametakiwa kuacha tabia  ya kutumia cheo chake kuomba rushwa ya ngono kwa Watendaji wa Vijiji katika Halmashauri hiyo na  kubadili mwenendo wake haraka iwezekanavyo. Onyo hilo limetolewa na  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa  wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.  Akizungumza na watumishi hao, Mary amesema, ni aibu kwa afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia maadili ya kiutumishi kutumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono toka kwa Watendaji wa Vijiji jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya kiutendaji katika utumishi wa umma. Amemtaka afisa huyo kuacha tabia hiyo na kujirekebisha maramoja ili awe mfano bora kwa watumishi anaowasimamia kimaadili. Pia amemtaka, a...

MRADI WA SOKO LA KISASA MANISPAA YA MOROGORO WAMKUNA DKT. KIJAJI

Image
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo, wakati akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo ndilo la mfano katika miradi ya kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato.  Muonekano wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo limekamilika kwa asilimia 30 na linatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali Septemba mwaka huu na kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 900. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kushoto) akietendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro  Mkoani Morogoro . (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango) ……………………….. Na Peter Haule, WFM, Morogoro Halmashauri zote nchini zimetakiwa kujifunza kutekeleza miradi ya Kimakakati inayopatiwa ruzuku na Serikali, katika Hal...

KATIBU MKUU NISHATI ASIFU WATAALAMU TANESCO

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua,(watatu kulia), akizungumza na vyombo vya habari mbele ya mashine (turbine) ya kufua umeme inayofanyiwa matengenezo makubwa ya kujilinda kwenye kituo cha kufua umeme wa gesi asilia cha Ubungo II, jijini Dar es Salaam. KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, amewapongeza wataalamu wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha umeme unawafikia wateja licha ya changamoto ambazo zinawakabili . Dkt. Mwinyimvua ametoa pongezi hizo leo Februari 26, 2019 wakati alipotembelea vituo vya kufua umeme wa gesi   vya Ubungo I, Ubungo II, Songas lakini pia kuona kazi ya kufunga transfoma mpya kwenye kituo kikuu cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo.   Dkt. Mwinyimvua ambaye alifuatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amesema “Tunazitambua changamoto zinazowakabili, lakini niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha hu...

Kuzaliwa Fatma Bint Muhammad (a.s) ndio siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani-Maulana Sheikh Jalala.

Image
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari katika kukumbuka kuzaliwa kwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Bi Fatma bint Muhammad (a.s), kuwa ndio Siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani, Jana Masjid Ghadir, Kigogo Post Jijini Dar es salaam Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwenu Nyote. Siku hii ya leo ambayo kwa tarekh ya Kiislamu tunaita ni Mwezi 9,ni siku ambayo wanazuoni wa Kiislamu wameitangaza kuwa ni Siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani, sababu kubwa ya Tangazo hilo nikutokana na kuzaliwa Bint ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae Bint huyu na Mama huyu na dada huyu ananafasi kubwa katika Dini ya Uislamu. Mama huyu ambae tunakumbuka mazazi yake ambae Maulamaa wameitangaza kuwa ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani daraja lake mama huyu katika Uislamu ni kama vile daraja la Maryam bint Imran, Mama yake Nabii Issa (a.s). Lakini kwanini kukumbukwa mama huyu lakini vilevile kwani ku...

SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAENDELEA KULINDA NA KUKUZA HAKI ZA BINADAMU -PROF KABUDI ALIAMBIA BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU LA UMOJA WA MATAIFA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akihutubia Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika jijini Geneva nchini Uswisi.  .................................. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu na ustawi wa jamii kama kipaumbele chake na  itaendelea kushirikiana na Baraza hilo kuhakikisha haki za binadamu nchini na duniani kote zinadumishwa. Prof. Kabudi amesema hayo alipolihutubia Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika jijini Geneva nchini Uswisi. Prof. Kabudi amesema Serikali ya Tanzania imelenga pamoja na mambo mengine kuimarisha haki za binadamu, utawala bora na utii wa sheria nchini na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu. “Serikali imelenga kuimarisha haki za binadamu, utawala bora, utii ...