Posts

VICHWA VYA HA BARI, MAGAZETI YA LEO 31 DESMBA 2016.

Image

EWURA YARIDHIA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME

Image
    MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017. Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake. Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme. Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi. Kundi laTIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano...

HALI YA UCHUMI WA TANZANIA JULAI – DESEMBA 2016.

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akielezea waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa uchumi wa nchi na mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya kiuchumi alipozungumza na wanahabari katika wizara hiyo leo jioni soma taarifa kamili ya waziri huyo hapa chini.  ...................................   Nashukuru kupata fursa ya kuzungumza nanyi  leo kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2016 na matarajio hadi Juni 2017. Nitajitahidi kutumia lugha rahisi ili wananchi wa kawaida waweze kuelewa mambo ya msingi kuhusu mwenendo wa uchumi wa nchi yetu. Ustawi wa Uchumi Unapimwaje? Ustawi wa uchumi wa Taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mbalimbali. Kwa kifupi, ustawi wa uchumi unapimwa kwa kuangalia kama shughuli mbalimbali za kiuchumi zinaongezeka au zinapungua au kama zimedumaa. Shughuli  muhimu zinazoangaliwa ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi; uzalishaji wa bidhaa za viwandan...