Rais wa REAT nchini Mwalimu Dauda Bilikesi akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba hawapo pichani akimuomba makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Isdor Mpango kukaa na wastaafu ili kutatua changamoto zao.
Na Alodia Babara- Bukoba
UMOJA wa wastaafu Tanzania (REAT) wamemuomba makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isidor Mpango kukutana nao sambamba na kuwakutanisha na viongozi,watendaji wa Serikali (waajiri)na mifuko ya Hifadhi ya jamii ili waweze kujadili hoja 13 walizowasilisha kwa Serikali.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Bukoba Rais wa REAT nchini Mwalimu Dauda Bilikesi amesema mwezi Januari mwaka huu umoja huo ulituma maombi kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake,watoto na makundi maalum na kuwasilisha hoja zao 13 mojawapo ikiwa ni kuboresha kima cha chini cha pensheni ambapo kwa mujibu wa sheria kima cha chini cha pensheni inapaswa isiwe chini ya asilimia 40 ya mshahara wa watumishi wa Umma.
"Wapo wastaafu wengi wanaolipwa kiasi cha shilingi 45,000 hadi 75,000 pungufu 100,000 kama pensheni ya mwezi,ndio hao wasio na huduma ya bima ya Afya chini ya mfuko wa NHIF kutokana na udogo wa pesheni zao huku umri wao mkubwa unasababisha kukabiliwa na maradhi ya mara kwa mara na ugumu wa maisha ya sasa, hivyo, kupitia hadhara hii tunamuomba mhe. makamu wa Rais Dkt. Mpango atupatie nafasi ya kukutana naye nakutusaidia kufikia muafa wa kutatatua changamoto zetu"amesema Bilikesi.
Amesema maombi yao yanakuja baada ya taarifa ya Naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu, ajira, kazi na Vijana Patrobasi Katambi aliyoitoa bungeni Septemba mosi mwaka huu ya kuwa Serikali imeboresha kima cha chini cha pensheni cha wastaafu wote kifikia shl 100,000 huku wengine wakiwa bado.
No comments:
Post a Comment