Leo tatehe 30/09/2022, ndio siku ya mwisho ya ziara ya Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir Bin Ally Nchini Uingereza ambapo ameweza kuitembelea miji mbalimbali na hasa yenye Waislaamu wengi Watanzania wanaoishi huko.
Jana tarehe 29/09/2023 akiwa katika Mji wa Leeds-Bangaladesh Center, aliweza kuwaaga diaspora wetu Nchini humo pamoja na wale wote walioshiriki katika Mkutano huo, ikiwa ni ishara ya ziara hiyo kufikia mwisho.
Inatajwa ni miongoni mwa ziara Bora kuwahi kufanywa na Viongozi wa kidini kutoka katika Mataifa ya kiafrika, na hii ni kwa sababu ya ujumbe aliokuwa nao kiongozi huyo Mkuu wa kidini Nchini Tanzania.
Ziara hiyo ilibeba ujumbe mzito kwa ulimwengu ikiwemo Amani kwa watu wote, uchumi, elimu, afya, chakula, teknolojia, usawa, haki na wajibu, maridhiano, mshikamano na umoja, uongozi na utawala bora pamoja utunzaji wa mazingira kwa kuvilinda viunbe hai.
Zaidi ya hapo, Mheshimiwa Mufti ameitumia ziara hiyo kwa kuwakumbusha Watanzania waishio katika Mataifa mengine (Diaspora) kuwekeza mitaji yao nyumbani ili iwe ni faida kwa Nchi na Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment