Sunday, September 17, 2023

RC MAKALLA AZINDUA MAJARIBIO YA CHANZO KIPYA CHA MAJI BUTIMBA, KUTATUA UHABA WA MAJI NYAMAGANA NA WILAYA TATU ZA MWANZA, 69BIL ZATUMIKA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla Septemba 15, 2023 amezindua Majaribio ya Chanzo Kipya cha Tiba ya Maji Butimba kituo ambacho kitazalisha Lita milioni 48 kwa Siku kilichojengwa na Kampuni ya Sogea Satom chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Akizungumza na wananchi baada ya kubonyeza kitufe na kuwasha mitambo ya Maji na hivyo kuanzisha rasmi majaribio Mhe. Makalla amesema katika muda mfupi ujao wananchi wanaoishi Nyamagana Katika maeneo ya Sahwa, Igoma, Kishiri, Wilaya ya Ilemela Nyamhongolo na Kisesa Katika Wilaya ya Magu na Usagara Katika Wilaya ya Misungwi wataanza kupata Maji kutoka katika chanzo hicho kilichogharimu zaidi ya bilioni 69.

Mhe. Mkuu wa Mkoa ametumia hafla hiyo kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili kutekeleza mradi huo unaotarajia kuongeza uzalishaji hadi lita milioni 138 kwa siku kutokana na chanzo cha sasa kuzalisha lita milioni 90 na miradi mingine inayolenga kuondoa kero ya Maji kwa wananchi Mkoani humo na wataalamu wote waliofanikisha ujenzi wa mradi huo.

Vilevile, Mhe. Makalla amebainisha kwamba kupitia mradi wa LVWATSAN kwa suluhisho la muda wa Kati tayari zabuni kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa mabomba na Matenki makubwa Sita yenye uwezo wa kuhifadhi maji jumla ya Lita milioni 31 imetangazwa na kwamba mkandarasi anatarajiwa kupatikana siku za usoni.

"Ndugu wananchi, napenda kuchukua fursa hii kuwaomba mnapoona maji yakivuja mtaani mtoe taarifa MWAUWASA nanyi mzishughulikie taarifa hizo kwa haraka na kwa umakini ili kuokoa maji, kuwatia moyo wananchi na kuzuia matatizo kama hayo yasijitokeze tena sehemu ileile." Mkuu wa Mkoa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, Mhe. Sixbert Jichabu amesema chama tawala kina matarajio makubwa kwa serikali yao na Mhe. Rais Samia ameamua kuwaletea huduma bora wananchi na ametoa pongezi kwa

Akiongea kwa niaba ya Wana Nyamagana Mhe Stanslaus MABULA Mbunge Jimbo la Nyamagana amemshukuru Rais wa awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kutoa zaidi ya Bilioni 69 za Mradi huo ambapo toka ameingia madarakani amekuta Mradi huo upo hatua ya awali Ya manununuzi Lakini kwa dhamira ya kumtua ndoo MWANAMKE kichwani ametoa fedha hizo. Mhe Mabula amesema, amehemewa na furaha nyingi kwa maji kuanza kuwafikia wanachi wa pembezoni mwa Nyamagana punde uzinduzi huo unapoanza.

Hafla Hiyo ya uzinduzi imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya NYamagana Mhe Amina Makilagi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Hassan, Mbunge Jimbo la Ilemela Mhe Angelina Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA Mhe Christopher Gachuma pamoja na Wajumbe wake, Kamati ya siasa Nyamagana ikiongozwa na Peter BEGA, Mwenyekiti wa CCM Imelema Yusuph Bujiku pamoja na Kamati za ulinzi na usalama Wilaya ya Ilemela, Nyamagana na Mkoa.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo La Nyamagana







No comments:

Post a Comment