Saturday, September 30, 2023

TOENI USHIRIKIANO KWA MIRADI YA TASAF- Ridhiwani Kikwete

 

Watumishi pamoja na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF)  ili kuwainua watu wenye uhitaji



Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaongea na wananchi wa kata ya Msata na Msoga katika mikutano baada ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).


Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya Msoga , na baadae kuona mafanikio ya miradi ya kuwezesha wananchi na miradi ya miundombinu ya jamii, 


Naibu Waziri aliwaomba wananchi na Halmashauri kuendelea kushirikiana na Miradi ya TASAF ili kuwanyanyua wananchi wenye uhitaji. 


Katika mkutano huo, Naibu Waziri aliwapongeza Halmashauri kwa kutenga pesa za kukopesha vikundi vya maendeleo vikiwemo vikundi vya wanufaika wa miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wameshukuru TASAF kwa jitihada za kuwakomboa katika hali mbaya ya umaskini na pia kuishukuru Halmashauri kwa kuendelea kutenga pesa kwa vikundi vikiwemo vya TASAF na mafanikio yanayoonekana ni kwa sababu ya mipango hii kufanywa pamoja. 

Halmashauri ya Chalinze imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali na katika mkutano huo pamoja na makundi mengine, vikundi viwili vya Pain For Success na Muungano ambavyo kila kimoja kilikopeshwa shilingi Milioni 10 vilitoa ushuhuda wa jinsi mipango hivyo ilivyofanikiwa kwa kuonyesha bidhaa mbalimbali walizotengeneza na miradi waliyoshiriki. 


No comments:

Post a Comment