Na Alodia Babara- Bukoba.
Watoto zaidi ya 85,000 wenye umri chini ya miaka nane wanatarajia kuchanjwa chanjo ya polio Halmashuri ya Wilaya ya Bukoba, kuanzia Septemba 21 hadi Septemba 24, Mwaka huu 2023
Mratibu wa chanjo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Yohana Baruba amesema hayo hivi karibuni, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wanalenga kuchanja watoto wenye umri chini ya miaka minane wapatao 85,795 kuanzia Septemba 21 hadi Septemba 24.
Yohana amesema, chanjo hiyo itatolewa nyumba kwa nyumba, mashuleni, makanisani, msikitini, vituo vya kutolea huduma za afya na katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima
amesema zoezi hilo ni la kitaifa na si dogo ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo inayotarajiwa kutolewa katika mikoa sita ya Tanzania ikiwemo Kagera.
"Tunapaswa kushirikiana wote kwa hili kuhakikisha tunafanikisha zoezi hilo ikitokea mtendaji yoyote akagoma kwenda kuhamasisha na kueleza umuhimu wa kupata chanjo hii kwa wananchi au kupotosha zoezi,tupate taarifa zake tutamchukulia hatua kwa muijbu wa sheria maana tukiendelea kuwalea na kuwafumbia macho watu wa aina hiyo ni kuliangamiza Taifa" amesema Siima.
Siima amesema baada ya zoezi hilo kumalizika watafanya tathimini kuona mafanikio na changamoto zilizojitokeza ikiwemo kuwabaini watakao kwamisha zoezi hilo.
amesema ni vyema matangazo yanayohusu umuhimu wa chanjo yaendelee kutolewa, ikiwemo kubandika mabango yanayozungumzia tukio hilo, kuwashirikisha viongozi wa dini waweze kutoa matangazo hayo kwenye nyumba za ibada maana hili ni zoezi muhimu kwa ajili ya kunusuru watoto wetu na janga hilo.
"Tumelenga kufikia asilimia 100 tunapaswa kuzidi asilimia hiyo hivyo tunapaswa kukemea upotoshaji wa aina yoyote mfano kuna watu wamekuwa wakitishia kuwa chanjo zina madhara tujipange wote kwa pamoja kukemea hayo.
No comments:
Post a Comment