Sunday, June 30, 2019

MAJI SAFI NA SALAMA CHANGAMOTO KWA WATOTO WENGI MASHULENI

Eng.Patrik Kibasa Mkurugenzi Souwasa


Joyce Joliga

Songea. Bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama katika shule za msingi hali ambayo inachangia watoto kunywa maji yasiyosalama kwa afya zao hivyo kujikuta wakiugua mara    kwa mara homa za matumbo,kuharisha ,UTI .

Tatizo la ukosefu maji safi na salama mashuleni limekuwa likiwasababishia adha wanafunzi wengi kwani baadhi wamejikuta wakishindwa kuhudhulia masomo kutokana na kuumwa   na wengine wamejikuta wakishindwa kufanya vizuri  kwenye masomo yao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa Juni 19 2019  kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mabilioni ya watu duniani wanaendelea kutaabika kutokana na kukosa huduma bora za maji na masuala ya usafi.

Ripoti hiyo imeainisha takwimu mpya zikionyesha kwamba mwaka 2017 watu bilioni 3 walikosa huduma za msingi kama sabuni na mahali pa kunawa mikono nyumbani , wakiwemo karibu robo tatu yao wanapatikana katika nchi zenye maendeleo duni.
Kila mwaka watoto 297,000 wa chini ya umri wa miaka mitano kufariki diunia kutokana na kuhara kunakochangiwa na ukosefu wa huduma za WASH. 

Kwa upande wake  Diwani kata ya Ruhuwiko Wilbert Mahundi , anasema tatizo la maji katika shule za msingi za kata yake ni kubwa na limechangiwa na baadhi ya shule kukatiwa maji na zingine kutokuwa na maji ya bomba  na zipo ambazo zinatumia  maji ya visima.

Anasema tayari ameziagiza kamati za shule  kujadili namna ya kuhakikisha upatikanaji wa  Vifaa vya kunywea maji wanafunzi na  kuwekea maji safi na salama shuleni ili kuweza kuwanusuru watoto dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu,tumbo ,taifodi na UTI

Anasema,Kamati hizo zijadili n .kamati za shule zimetakiwa kujadili namna ya kuhakikisha upatikanaji wa  Vifaa vya kunywea maji wanafunzi na  kuwekea maji safi na salama shuleni ili kuweza kuwanusuru watoto dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu,tumbo ,taifodi na UTI amna bora na kupeleka maazimio yao kama agenda kwenye vikao vya baraza la Kata ilizijadiliwe na kupelekwa kwenye vikao Vya baraza la madiwani zijadiliwe na kupangiwa bajeti kwa ajili ya utekelezaji huo
Aidha ,amewataka walimu wakuu na maafisa Elimu Msingi na sekondari waangalie changamoto za upatikanaji wa bili za maji ili ziingizwe kwenye capitation na kwa ajili ya kupata fedha za kulipia ili kuweza kukwepa adha ya kukatiwa  maji mara kwa mara na kuwasababishia watoto kukosa maji safi na salama shuleni.
" Huduma ya maji safi na salama ni muhimu kwa watoto wetu ilikuweza kuwaepusha na milipuko ya magonja ya kipindu pindu ,homa za matumbo,UTI na hivyo tunapaswa kuwalinda na kuwasaidia wakiwa shuleni,"Alisema Mahundi
Aidha amewataka wazazi kupitia kamati na Bodi za shule kusimamia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na Vifaa vya kutunzia maji na vikombe Vya kunywea maji badala ya kutumia mikono
Kwa upande wake Mwanafunzi Fatuma Ally wa shule ya Msingi Ruhuwiko anasema kwa sasa wanafunzi hawapati maji safi kwani yamekatwa na hakuna vikombe vya kunywea maji hivyo wanatumia mikono pia hakuna utaratibu mzuri wa upatikanaji maji safi shuleni hapo hivyo ameuomba uongozi wa shule kuwasaidia wanafunzi wakiwa shule kupata huduma hiyo ilikuwaepusha na maradhi ya kuharisha na kuumwa ugonjwa wa matumbo.
Naye Ibrahim Hyella mkazi wa Ruhuwiko amepongeza jitihada ambazo zimeanza kuchukuliwa na  kamati ya shule kwa kushirikiana na Diwani huyo kuwa zitasaidia watoto kupata maji safi na salama na hivyo kujikinga na maradhi ya mlipuko.

Mamlaka imetumia kiasi cha Tshs 117,448,700.00 kwa ununuzi wa bomba chache, viungio vya bomba na gharama za uchimbaji naulazaji bomba kutoka kwenye mapato yake ya ndani ili kuwafikia wateja wengi waliokuwa hawapati huduma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafina Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa,amesemawateja hao wameweza kuunganishwakatika kipindi kifupi kwa kuwa Mamlaka ilitoa punguzo maalumu kwa wateja ili kuweza kujiunga kwa gharama nafuu kisha kuendelea kulipia gharama za maunganisho zilizobaki kwa makubaliano maalumu ya kulipia katika kipindi cha miezi sita kwa kuwa huduma ilikuwa imekwisha fika katika maeneo yao.Hii ni katika kuhakikisha wananchi wote wa Manispaa ya Songea wanapata huduma ya majisafi inayotolewa na SOUWASA kwa kuangalia kipato halisi cha Mtanzania.

Mkurugenzi Mtendaji aliongezea kufafanua kuwa Serikaliya awamu ya tano imedhamiria kumtua mama ndoo ya maji kichwani hivyo Mamlaka inahakikisha wakazi wa Manispaa ya Songea wanapata huduma ya majisafi na salama uhakika.

Katika kipindi hicho cha muda mfupi, Mamlaka imeweza kuwafikia wananchi ambao maeneo yao hayakuwahi kupata huduma ya majisafi kwa kuwaunganisha kwenye mtandao wa majisafi nakuweza kuondokanana kero ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji au kutumia maji yasiyo salama ambayo yaliwasababisha magonjwa mbalimbali yaliyotokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.

Mhandisi Patrick Kibasa amesema, wateja hao wameunganishwa kati ya Julai naDesemba 2018. Lengo ni kutoa huduma kwaasilimia 95 ifikapo mwaka 2020na kwa sasa huduma hiyo inatolewakwa asilimia 80 kwa kata za mjini zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea.

Ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unakua endelevu katika Manispaa ya Songea Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa Mamlaka inahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatunzwa. Mpaka sasa jumla ya miti 2,500 imepandwa katika bonde la mto Luhira na takribani zaidi ya miti 5,000 inategemewa kupandwa katika vyanzo vya mlima Matogoro katika kipindi hiki cha masika.
  zikiwemo shule  na taasisi mbalimbali

No comments:

Post a Comment