KILOSA YAANZA MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA EL NINO - DC SHAKA APIGA MARUFUKU MAFUNZO, AAGIZA FEDHA ZINUNUE VIFAA VYA DHARULA
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka ameongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Maafa ya Wilaya kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama na wadau mbalimbali kujadili maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Akifungua kikao hicho, Mhe. Shaka amesema Wilaya ya Kilosa imejifunza kutokana na athari za mafuriko ya miaka ya nyuma na safari hii maandalizi yote yatajikita kwenye vitendo, sio kwenye makaratasi. Amefafanua kuwa uamuzi huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza mikoa na wilaya zote kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha taarifa za TMA hazibaki kwenye makaratasi bali zinafuatwa na hatua za vitendo. Akizungumza kwa msisitizo, DC Shaka alisema: _"Wilaya ya Kilosa tumeamua fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya maafa zitanunua vifaa vya dharura vinavyoonekana. Sitaki kusikia mafunzo, semina na w...