TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA
TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Tanzania International Tourism Festival (TITF) imeandaa tamasha la Sanaa za ufundi litalalofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 11 Oktoba jijini Arusha. Tamasha hilo linalenga kuunganisha Sanaa, Ufundi, Utamaduni, Utalii na Uchumi wa Ubunifu, pamoja na kutoa fursa za masoko, biashara na uwekezaji kwa wazalishaji wa bidhaa za Sanaa na ufundi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Edward Buganga alisema TITF imezishirikisha BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania na COSOTA katika maeneo yanayohusiana na majukumu yao. Alisema tamasha hilo litafanyika katika Viwanja vya General Tyre, Njiro, Arusha. Alisema BASATA itashiriki katika maeneo yanayohusu maendeleo na ukuzaji wa sanaa, wasanii na wadau wa sanaa, pamoja na kuhamasisha fursa zinazotokana na uchumi wa ubunifu. Buganga alisema Bodi ya Filamu Tanzania itashiriki katika maeneo yanayohusu tasnia ya filamu na ...