Posts

DKT. MPANGO AWASILI COMORO.

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo wa Comoro Mhe. Houmed Mssaidie mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim uliopo Moroni nchini Comoro tarehe 25 Mei 2024. Makamu wa Rais anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uapisho wa Rais Mteule wa Comoro Azali Assoumani unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mei 2024. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim uliopo Moroni nchini Comoro tarehe 25 Mei 2024. Makamu wa Rais anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uapisho wa Rais Mteule wa Comoro Azali Assoumani unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mei 2024. (Kulia ni Waziri wa Kilimo wa Comoro Mhe. Houmed Mssaidie na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu) Makam...

NAWASHUKURU KWA DUA ZENU - DK.MWINYI

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj  Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Wazee wa Vijiji vya Ukongoroni na Charawe kwa kumuombea dua baada ya kukamilika barabara ya  Ukongoroni hadi Charawe na kuipongeza Serikali. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa na dua ya kumuombea iliyoandaliwa na Wazee wa Ukongoroni na Charawe iliyofanyika Ukongoroni, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja tarehe: 24 Mei  2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea dua nchi ili Mwenyezi Mungu aidumishe katika amani na kutimiza ahadi za maendeleo kwa wananchi.  

SOME AANZA KUWATETEA WANAFUKAYOSI.

Image
  MRISHO SOME Diwani wa Kata ya Fukayosi, akisalimiana na mmoja wa Madiwani baada ya kuapishwa rasmi kuwa diwani. Picha na Omary Mngindo. Mrisho Some akila kiapo. Picha na Omary Mngindo. Mrisho Some (kushoto pichani) diwani mpya Kata ya Fukayosi akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo ikiwa ni mara yake ya kwanza. Picha na Omary Mngindo. ................................... Na Omary Mngindo, Bagamoyo. DIWANI mpya wa Kata ya Fukayosi halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani  Mrisho Some ameanza kuwapigania wakazi wake, kwenye baraza lake la kwanza kuanza kutekeleza majukumu yake. Some alianza kazi hiyo katika Baraza la robo ya tatu ambapo alianza kwa kuiomba TARURA wilaya hiyo kuiangalia barabara itokayo Kijiji cha Fitina haina Posho kuelekea shule ya sekondari ya fukayosi. Akiwa katika kikao hicho Some alisema kwamba ndani ya Kata hiyo kuna changamoto kadhaa huku akianza na barabara kutokea Fitina haina Posho kuelekea shuleni huko. "Mhesh...

MWENGE WA UHURU WATUA LINDI, KUTEMBELEA MIRADI 53

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo, Mei 24, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa  mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ambapo unatarajiwa kuwekwa mawe ya msingi, na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 45.9 Makabidhiano ya Mwenge huo  yamefanyika katika viwanja vya Ndege Wilayani Kilwa Mkoani Lindi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali sambamba na wananchi wa maeneo hayo. Akitoa taarifa ya Mkoa wakati wa Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru, Mhe Telack amesema kuwa katika Mkoa wa Lindi Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 45.9 Akipokea Mwenge huo Telack amesema Mwenge huo wa uhuru ukiwa Mkoani Lindi unatarajiwa kukimbizwa kwa umbali wa kilometa 1128.7 katika Wilaya 5 na halmashauri 6 za Mkoa huo ambapo jumla ya miradi 15 itawekwa mawe ya msingi, miradi 13 itazinduliwa na miradi 25 itatembelewa. Telack amesema kwa k...

UMARUKI WATUMIA MILIONI 7, KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO PWANI.

Image
  Viongozi wa Umoja wa Maendeleo wa Watu wa Rufiji mkoani Pwani na Kilwa mkoani Lindi (UMARUKI) waishio Morogoro, wakikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani ambao umepokelewa na Katibu tawala mkoani Pwani (RAS)  Rashid Mchata kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo. .................................... Na Rashid Mtagaluka, Kibaha. Umoja wa Maendeleo wa Watu wa Rufiji mkoani Pwani na Kilwa mkoani Lindi (UMARUKI) waishio Morogoro, jana Mei 23/2024 umekabidhi msaada wa nguo kwa wananchi waliopatwa na athari ya mafuriko mkoani Pwani. Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa wa Pwani, Katibu Mkuu wa UMARUKI Bwana Juma Mtumbei alisema umoja huo umeguswa na tukio hilo, hivyo kama binadamu wameona wanao wajibu wa kuwasaidia. Kwa mujibu wa Mtumbei, msaada waliotoa kwa waathirika hao ni pamoja na nguo za watoto, wanawake, wanaume pamoja na nguo maalumu za kujistiri wakati wa baridi zote zikiwa na  thamani ya shilingi Milioni Saba na laki saba. Kwa upan...

MAJALIWA: TUMEDHAMIRIA KUONGEZA KIPATO CHA WANANCHI

Image
  Asema lengo ni kuleta uwiano mzuri wa kiuchumi na kijamii mijini na vijijini WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya imedhamiria kuongeza ushiriki wa wananchi katika kujenga uchumi wa viwanda, kuongeza kipato kwa wananchi wengi na kuleta uwiano mzuri wa kiuchumi na kijamii mijini na vijijini. “Ili kufikia lengo hilo, Serikali inatekeleza Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini kwa kufanya mapitio na maboresho ya sera, sheria na kanuni ambazo zinakuwa ni kikwazo katika ufanyaji wa biashara nchini.” Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 23, 2024) kwenye ufunguzi wa Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji baina ya Uganda na Tanzania, katika Hoteli ya Johari Rotana jijini, Dar-es-Salaam. Amesema Serikali imeimarisha utoaji huduma kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki 55 ya taasisi 50, pia sheria 13 zimeshafanyiwa marekebisho ili kupunguza au kuondoa kodi, ada na tozo na kupunguza au kuweka misamaha ya ushuru wa forodha. “M...

JKT RUVU WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA SEKTA YA UTALII.

Image
  Kanali Peter Mnyani (Mwenye suti) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John wakifunua kitambaa kuashiria kuzinduliwa kwa zuu hiyo. Picha na Omary Mngindo. .................................... Na Omary Mngindo, Ruvu. JESHI kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, imeunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Saluhu katika suala la kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo vikiwemo vya wanyamapori kupitia sekta ya utalii. Hatua hiyo inatokana na kambi ya Ruvu kuanzisha kitalu cha kuhifadhia wanyama hao, kwa kutenga ardhi yenye ukubwa wa eka 70, pembezoni mwa kambi wakianza na Twiga, Swala, Pundamilia na wengine wadogowadogo. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kikosi hicho Kanali Peter Mnyani, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John, wakati wa uzinduzi wa zuu hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanajeshi wastaafu na mamia ya wananchi. "Mkuu wa Wilaya uanzishwaji wa zuu ya wanyama tunalenga kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu, ambae ...