Posts

MAKONDA ATOA MAAGIZO KWA MAWAZIRI, KAGERA

Image
  Na Alodia Babara  Bukoba.  Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Paul Makonda,  ametoa maagizo mbalimbali kwa Mawaziri wa wizara nne hapa nchini ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapigia simu mawaziri hao na kutoa majibu ya changamoto na kutatua changamoto hizo. Mawaziri waliopigiwa simu ni pamoja na waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Waziri wa mambo ya ndani Hamad Massaun, waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa. Makonda ametoa maagizo hayo leo Novemba 9, 2023 wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara akiongea na wananchi mkoani Kagera uliofanyika uwanja wa mashujaa Mayunga. Moja ya changamoyo zilizotajwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu, kingo za mto Kanoni, ujenzi wa stend kuu, uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Bukoba, tatizo la nida maeneo ya mipakani na ujenzi wa barabara za lami. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa akijibu kuhusu...

HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAVUKA MALENGO UKUSANYAJI WA MAPATO

Image
  Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imevunja rekodi ya kukusanya kiwango katika kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 kuaniza Julai mpaka Septemba 2023 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya Bagamoyo Mhe. Halima Okashi katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo tarehe 09 Novemba 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya. Akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza Madiwani na Watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 kuanzia Julai mpaka Septemba 2023.  Katika kipindi hicho Halmashauri imekusanya zaidi ya shiling bilioni 1 sawa na asilimia 27.7 ambapo ni asilimia 2.7 zaidi ya malengo waliyojiwekea ya asilimia 25. "Niwapongeze Madiwani wa Kata zote pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Bagamoyo kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato kwenye taarifa yenu inaonyesha mapato yaliyopatikana ni asilimia 27.7 ambapo malengo yalikuwa ni asil...

MAGAZETI YA LEO TAREHE 09 NOVEMBA 2023.

Image
 

WANUFAIKA MRADI WA KLIC WATAKIWA KUTUNZA VIFAA VYA TEHAMA-TET

Image
  Na Andrew Chale,Dar es Salaam. Shule zote nchini zilizonufaika na vifaa vya mradi wa KOREAN E-LEARNING IMPROVEMENT COOPORATION(KLIC) ulio chini ya Ofisi ya Elimu ya Gwangju Metropolitan ya nchini Korea ya Kusini, wenye lengo la kuboresha elimu nchini katika eneo la TEHAMA, wametakiwa kuhakikisha wanatumia vizuri , kiusahihi na kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kunufaisha wanafunzi wengi zaidi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utafiti,Habari na Machapisho waTaasisi ya Elimu Tanzania(TET), Bw. Kwangu Masalu leo tarehe 8/11/2023 katika shule ya Sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika ziara ya ujumbe wa watu kutoka korea ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya kugawa vifaa vya TEHAMA vya kujifunzia masomo pamoja na kutoa mafunzo ya vitendo ya namna ya kuvitumia kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo . Mwakilishi wa walimu waliopo kwenye ziara hiyo kutoka nchini Korea Kusini, Bwana.Kim Chi Gon ameeleza kuwa , wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha...

WAFANYABIASHARA MKURANGA, KIBITI WAMSIFU SAMIA UHURU WA BIASHARA.

Image
  Na Mwandishi Wetu, Mkuranga WAFANYABISHARA wilayani Mkuranga na Kibiti, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuliza dhorobu ya hali ya biashara nchini. Wamesema kwenye wilaya hizo biashara zinafanyika kwa amani na utulivu bila usumbufu tofauti na miaka ya nyuma. Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye mkutano kati ya wafanyabishara wa wilaya hizo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) inayoendelea mkoani Pwani yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabishara. Mfanyabiashara Hassan Mbwana Kambangwa, amesema wafanyabiashara kwa asilimia kubwa wilayani humo wananufaidika sana tangu kuingia kwa utawala wa Rais Samia. Amesema "Kimsingi namshuruku Rais Samia kwa kutuletea ugeni uliotupa fursa ya kuzungumza changamoto zinazotukabili, lakini sisi tangu kuingia kwa utawala huu wa Mama Samia tunafaidika nao kwa asilimia kubwa." Mfanyabiasha huyo ametolea mfano wa mambo wanayofaidika nayo kuwa ni mikopo, uhusiano mazuri na halmashauri lakini pi...

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA BAGAMOYO LAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA CHA ROBO MWAKA 2023

Image
  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo tarehe 8 Novemba 2023 limekutana na kufanya Kikao chake cha kwanza katika mfululizo wa vikao viwili vya Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, vikao ambavyo vimepangwa kufanya tarehe 8-9 Novemba 2023. Katika Kikoa hicho Baraza lilipokea Taarifa za Utendaji kwenye ngazi ya Kata kwa robo ya kwanza ya mwaka 2023. Akipokea taarifa hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mohemed Usinga aliwapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote kwa kazi nzuri walizozifanya katika kipindi hiki cha robo ya kwanza. Aidha Mwenyekiti huyo aliagiza Madiwani pamoja na watendaji wa kata zote kutoanzisha miradi mipya ya maendeleo mpaka miradi iliyopo ikamilike, "Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji wa Kata hakikisheni mnamaliza miradi yote iliyokuwa haijakamilika kabla ya kuanzisha miradi mingine, tuhakikishe kwenye kata zetu tunamaliza viporo vyote vya miradi inayoendelea" alisema Mhe Usinga Nae Kai...

ZAIDI YA WANAFUNZI 2,000 WANUFAIKA NA MRADI WA CAMFED CHALINZE.

Image
  Zaidi ya wanafunzi 2,000 wasichana wamenufaika na Mradi wa Kampeni ya Elimu kwa mtoto wa kike (CAMFED) Halmashauri ya Chalinze kuanzia mwaka 2016 hadi sasa. Mkuu wa Kitengo cha Shule ya Sekondari, Madam Salama Ndyetabura akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Timu na Watoto wa Kampeni ya Elimu kwa Wanawake (CAMFED), katika mada iliyowasilishwa leo Tarehe 08 Novemba 2023, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chalinze. Madam Ndyetabura wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa CAMFED, alifafanua historia ya CAMFED katika Halmashauri ya Chalinze, Wanafunzi wakisaidiwa na CAMFED, CAMA network, miradi ya CAMFED katika Halmashauri ya Chalinze, Serikali na Ushirikiano wa CAMFED kusaidia elimu ya wasichana Chalinze. Madam Ndyetabura aliendelea kueleza kuwa CAMFED Tanzania ilitekeleza miradi mingi ya kusaidia elimu ya mtoto wa kike na wanawake vijana kama msaada wa elimu ya Msichana, mradi ambao ulianza 2016 hadi sasa na kusaidia jumla ya wanafunzi 2,3...