DC MTANDA ASITISHA ZABUNIMPYA YA WAKANDARASI WANAOZOA TAKA HADI KUFANYIKA KWA TATHIMINI .
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo jijini Arusha . ************************** Julieth Laizer ,Arusha Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amesitisha zabuni mpya ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu iliyokuwa ianze agosti mosi mwaka huu hadi kufanyika kwa tathimini baada ya kuwepo tuhuma kuna waliopewa zabuni hawana sifa. Mtanda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na ambapo alisema kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali juu ya wakandarasi hao kusitisha zoezi la ukusanyaji taka kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kujua hatma yao kutokana na kuambiwa mikataba yao imeisha. “Mimi malalamiko hayo niliyapata na ninachotaka kusema hapa ni kuwa nawaomba wakandarasi wote waliokuwa wanazoa taka waendelee na shughuli zao za uzoaji taka kama kawaida hadi pale watakapofanyiwa tathmini kila mmoja na kuweza kupewa ...