Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo jijini Arusha .
**************************
Julieth Laizer ,Arusha
Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amesitisha zabuni mpya ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu iliyokuwa ianze agosti mosi mwaka huu hadi kufanyika kwa tathimini baada ya kuwepo tuhuma kuna waliopewa zabuni hawana sifa.
Mtanda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na ambapo alisema kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali juu ya wakandarasi hao kusitisha zoezi la ukusanyaji taka kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kujua hatma yao kutokana na kuambiwa mikataba yao imeisha.
“Mimi malalamiko hayo niliyapata na ninachotaka kusema hapa ni kuwa nawaomba wakandarasi wote waliokuwa wanazoa taka waendelee na shughuli zao za uzoaji taka kama kawaida hadi pale watakapofanyiwa tathmini kila mmoja na kuweza kupewa mikataba mipya ila kwa sasa hivi nawaombeni mndelee na shughuli zenu kama kawaida.”amesema.
Mtanda amesema kuwa,kutokana na kuwepo kwa malalamiko mbalimbali ni lazima wakae chini wafanye tathmini ya utendaji kazi wa wakandarasi hao kipindi cha nyuma kama walifanya vizuri na kama kweli wanakidhi vigezo vya kuendelea na mchakato huo wa uzoaji taka kisheria na sio vinginevyo.
“Nitamwandikia Mkurugenzi wa Jiji barua kutaka zoezi hilo na barua hizo zisitishwe na ifanyike tathmini ya kina juu mkandarasi gani alifanya kazi nzuri,yupi aliyelipa fedha ya serikali inavyotakiwa,na wapi hawakufanya vizuri kwa mwaka huo uliopita na yupi bado anadaiwa fedha na serikali na tathmini hiyo itafanywa na kamati ya pamoja katika idara ya manunuzi ya jiji,idara ya mazingira ya jiji ili haki iweze kutendeka sitaki mambo ya ujanja katika hili “amesema Mtanda.
Ameongeza kuwa, kata ambazo zitaondolewa wakandarasi baada ya tathimini ni zile ambazo zimegundulika kutofanya vizuri na hawataweza kuendelea tena hakuna biashara za kueleana katika hilo,watakaoendelea na zoezi hilo ni wale waliofanya vizuri na wenye magari ya taka ili waendelee kuwekeza ,hivyo manung’uniko yote yakitolewa ndo mikataba mipya itatolewa na watu kuendelea na kazi katika maeneo yao waliyoomba na sio vinginevyo.
Aidha ameagiza maafisa tarafa wote kuleta orodha ya wakandarasi ambao hawajakusanya taka taka katika kipindi hiki kwa sababu za kutokuwa na uhakika kama watapatia mikataba mipya au lah kwani kwa kufanya hivyo ni kuhujumu juhudi za serikali za usafi wa mji na mazingira.
“Unajua kilichofanyika na jiji la Arusha ni kutoa barua la kusudio la kuingia mkataba rasmi ya wazoa taka katika maeneo mbalimbali,na wakiweka kusudio hatua inayofuata ni kusaini mikataba maalumu kwa ajili ya kuendelea na kazi hizo kila mmoja katika eneo aliloomba baada ya kukidhi vigezo Sasa nasitisha zoezi hilo la utoaji mikataba hadi tathmini ifanyike na kila mmoja ajiridhishe.”amesema Mtanda.
Aidha Mtanda ametoa wito kwa wazoa takataka wahakikishe wanaweka turubali ya kudhibiti taka zisimwagike na wataoenda kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria .
No comments:
Post a Comment