BENKI KUU YAONYA MATUMIZI MABAYA YA NOTI.
Hivi karibuni kuimeibuka wimbi la vitendo vya matumizi mabaya ya noti katika shughuli mbalimbali za kijamii hususan kwenye sherehe za harusi ambapo watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuziviringisha katika maumbo mbalimbali na kutumia kama mapambo, kuweka kwenye mwili wa mtu ulio loa jasho na matukio yote yanayofanana na hayo. Matendo haya yanatweza fedha ya Tanzania ambayo ni moja ya tunu za taifa letu.Vitendo hivyo vinaendelea kutokea licha ya Benki Kuu ya Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati tofauti kuvikemea. Hivyo basi, Benki Kuu ya Tanzania inatoa onyo kwa wananchi ambao bado wanakaidi onyo hili ambalo limetolewa mara kadhaa kuhusu namna sahihi ya kutunza noti za Tanzania zinazokuwa mikononi mwao kwa kuzitumia kinyume na maadili pamoja na matakwa ya kisheria. Kwa taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzan...