Posts

MGALU ASEMA, WANAWAKE NI JESHI KUBWA.

Image
  Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, (kulia) wakijadili jambo wakati wa maadhimisho ya Umoja wa Wanawake yaliyofanyika kiwilaya katika Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo.   Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, akizungumza katika maadhimisho hayo. ................................  Na Shushu Joel, Chalinze. NAIBU Waziri wa Nishati Subra Mgalu ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (UWT) kupitia mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini zaidi kwa kuwa wao ni jeshi kubwa na lenye uwezo wa hali ya juu. Akizungumza katika maadhimisho ya Umoja wa Wanawake kiwilaya yalivyofanyika katika Jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, alisema kuwa wanawake wamekuwa ni tegemeo kwenye ufanikishaji wa mambo mbalimbali ya kijamii . "Wanawake ni jeshi kubwa na lenye kutegemewa kwenye chama na serikali hivyo kinamama tuongeze uaminifu kwenye jamii zetu ili tuzidi kuendelea kuwa nguzo zaidi" Alisema Mgalu. Aidha amewapongeza kin...

KIKWETE NI JEMBE LINALOLIMA KIANGAZI NA MASIKA: UWT.

Image
Na Shushu Joel, chalinze. Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wamempongeza mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete kwa Utendaji wake wa kazi katika jimbo hilo. Kwa kawaida wakulima walio wengi hapa nchini hutumia muda mwingi katika shughuli ya kilimo kwenye kipindi cha masika lakini Mbunge wa Chalinze amekuwa akilima masika na kiangazi. Maneno hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Bagamoyo, Bi. Rukia Masenga, alipokuwa akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Umoja huo ambayo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji Cha Msoga, halmashauri ya chalinze. "Mbunge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika taifa hili kutokanana na jinsi alivyosimamia maendeleo makubwa katika jimbo lake na sisi Umuiya ya Wanawake ndani ya wilaya hii tumeridhishwa na utekelezaji wa ilani katika Jimbo lake "Alisema Bi Rkia. Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la chalinz...

OMARI MGUMBA AKEMEA KILIMO KUFANYWA ADHABU SHULENI.

Image
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba akizungumza na watumishi wa Halamashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah ..................................... NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa, wanachukia kilimo. Mgumba alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kulima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu. Alisema hapana, suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni uti wa mgongo laki...