NDALICHAKO ASAIDIA SHULE YA NYAMPAKU, RUFIJI.
Na Omary Mngindo, Muhoro WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Profesa Joyce Ndalichako, kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA, ameipatia shule ya Msingi ya Kijiji cha Nyampaku sh. Mil. 60, kujenga vyumba vitatu vya madarasa shuleni hapo. Shule hiyo iliyoko ndani ya Kata ya Muhoro wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, awali ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa, hali iliyowalazimu wanafunzi kuingia darasani kwa zamu. Akizungumza na Majira shuleni hapo, Mwalimu Mkuu Abdallah Simba alisema kuwa, mafanikio hayo yametokana na yeye kumwelezea Waziri Ndalichako, kuhusiana na changamoto hiyo, ambapo alimuunganisha na Mkurugenzi wa TEA ambaye ameiwezesha shule kupata kiasi hicho cha fedha. "Waziri Ndalichako alifika nikamwelezea changamoto ya vyumba vya madarasa, akaniunganisha na Mkurugenzi wa TEA aliyetusaidia shilingi milioni 60 tulizojenga vyumba vitatu, tumekarabati darasa moja, tumechimba vyoo sanjali na kisima cha maji," alisema Mwali...