TIMU YA PERA YACHUKUA USHINDI CHALINZE.
Mashindano ya Mazingira Kabumbu Cup 2017 Bagamoyo yamemalizika jana Tarehe 29 Oktoba katika mchezo wa fainali uliochezwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Msata Halmashauri ya Chalinze kati ya Pera na Bwilingu. Katika mechi hiyo ya fainali timu ya Pera imeibuka na ushindi wa goli moja dhidi ya Bwilingu na kuifanya timu ya Pera kuchukua Kombe la Mazingira Kabumbu Cup 2017 pamoja na zawadi ya Pikipiki ya Miguu mitatu. Gori hilo la Pera limefungwa dakika ya 72 na mchezaji Hassani wazri ambae aliingia kipindi cha pili. Muanzilishi wa Kombe hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, alisema lengo la mashindano hayo ni kuifanya jamii iwe na hamasa katika swala la kufanya usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika agizo lake la kutaka usafi wa mazingira ufanyike nchi nzima. Fainali ya kwanza ilifanyika katika Halmashauri ya Bagamoyo ambapo timu ya Nianjema ilitoka na ushindi ambapo nao walichukua ko...