Posts

MAGAZETI YA LEO TAREHE 27 SEPTEMBA 2017.

Image

WAZIRI WA AFYA ATOA MIEZI 8 KILA HOSPITALI YA MKOA NA WILAYA KUJENGA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA.

Image
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Umy Mwalimu ametoa miezi nane   kwa hospitali za mikoa na wilaya nchi nzima kuhakikisha wananjenga majengo ya kulea huduma za dharula katika hospitali hizo. Waziri ummy Mwalimu ametoa agizo hilo mjini Bagamoyo, tarehe 25 Septemba 2017, alipokuwa akiweka jiwe la msingi jengo la huduma za dharula na jengo la wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo. Alisema wananchi wengi wanafariki kabla ya kufika kwa Daktari kutokana na kutokuwepo kwa majengo yanayotoa huduma za dharula katika Hospitali hizo. alisema anatoa agizo hilo kuhakikisha kila Hospitali ya mkoa na Wilaya inaanza ujenzi wa majengo hayo na mwisho ni tarehe 30 juni 2018 kila Hospitali iwe imekamilisha ujenzi huo. Ujenzi wa majengo ya huduma za dharula na wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo umefadhiliwa na Taasisi ya Dhi nureyn na kwa kushirikiana na wahisani kutoka saudi Arabia  Aidha, ujenzi huo ambao utagharimu shilingi milio...

DKT.KIGWANGALLA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA MKURANGA

Image
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani. Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo. Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya. Awali wakati wa kukabidhi gari hil...

MWAKYEMBE ATAKA MKANDARASI MPYA WAKUTOA TIKETI UWANJA WA TAIFA.

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akisalimiana na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiongea na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiangalia eneo la uwanja wa mpira wa miguu akiwa na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.   PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM  ................................................. Na Benedi...