Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Umy
Mwalimu ametoa miezi nane kwa hospitali
za mikoa na wilaya nchi nzima kuhakikisha wananjenga majengo ya kulea huduma za
dharula katika hospitali hizo.
Waziri ummy Mwalimu ametoa agizo hilo mjini Bagamoyo, tarehe 25 Septemba 2017, alipokuwa akiweka jiwe la msingi jengo la huduma za dharula na jengo
la wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Alisema wananchi wengi wanafariki kabla ya kufika
kwa Daktari kutokana na kutokuwepo kwa majengo yanayotoa huduma za dharula
katika Hospitali hizo.
alisema anatoa agizo hilo kuhakikisha kila
Hospitali ya mkoa na Wilaya inaanza ujenzi wa majengo hayo na mwisho ni tarehe
30 juni 2018 kila Hospitali iwe imekamilisha ujenzi huo.
Ujenzi wa majengo ya huduma za dharula na wodi ya
wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo umefadhiliwa na Taasisi ya Dhi
nureyn na kwa kushirikiana na wahisani kutoka saudi Arabia
Aidha, ujenzi huo ambao utagharimu shilingi
milioni mia tani unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.
Wakati huohuo Waziri Ummy Mwalimu alisema
amekipandish hadhi kituo cha Afya cha msoga na kuwa Hospitali na kwamba
kilichobaki ni kukabidhi rasmi Barua ya kupandisha hadhi kituo cha Msoga.
Awali Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj, majid
Mwanga alimuomba Waziri wa Afya, kukipandisha hadhi kituo cha afya ili iwe
Hospitali kutokana na kukuwa kwa mji wa Chalinze.
Mkuu wa wilaya pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt. john Magufuli kwa kukabidhi majengo
yaliyokuwa yanatumika na Tan Roads huko msata ili yatumike kwa Halmashauri ya
Chalinze.
Alisema kutokana na kufunguliwa kwa Barabara ya Msata
Bagamoyo majengo ayo wanakusudia kufanya kituo cha Afya ambacho kitawahudumia
wananchi wa Msata na wapita njia.
Waziri Ummy Mwalimu pia amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kutafuta wafadhili waliofanikisha
ujenzi wa majengo ya huduma za dharula na wodi ya wazazi.
Watendaji kutoka Dhi
nureyn, Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Bagamoyo wakifuatilia shughuli ya uwekaji jiwe la msingi katika majengo ya wodi ya wazazi na jengo la huduma za dharula katika Hospitali ya Wilaya bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj, majid Mwanga akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment