Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi
gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo
vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.
Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya
Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge
wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya
Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa
ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo.
Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika
Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na
uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya
maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya.
Awali wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo
limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja
na Mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa
uangalifu wa hali juu huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika
kusaidia wananchi wake.
“Nimesikia kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine
ya X-Ray na na vifaa vingine muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na
tunawaomba muwe na imani na Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya
jambo hilo.
Hospitali ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa
vifaa ikiwemo mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati
akizungumza na wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali
katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment