Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi (kushoto akipokea msaada huo kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Jaji Paul Gwembe.
..................................................
NA
HADIJA HASSAN. LINDI
Mahakama
kuu kanda ya Mtwara, Jamii ya watu wa kusini (SEDO) waungana na wadau wengine
wa maendeleo kuwasaidia waathirika wa Mafuriko Mkoani Lindi kwa kutoa pesa
taslimu na vitu mbali mbali vyenye thamani ya Shilingi milioni 8,637,000.
Misaada
hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Godfrey
Zambi ofisini kwake.
Misaada
hiyo ni pesa taslimu shilingi milioni 3.1 kutoka Mahakama kuu kanda ya Mtwara,
Nguo mifuko tisa,mabati 250 yenye thamani ya shilingi milioni 4, pamoja na unga
viroba 15 vyenye ujazo wa kg 25 na sukari mifuko 8 ya kg 25 vyenye thamani ya
shilingi lako 537,000 kutoka kwa jamii ya watu wa kusini (SEDO).
Akikabidhi
msaada huo Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Jaji Paul Gwembe alisema
kuwa fedha hizo walizokabidhi ni michango kutoka kwa watumishi wa Mahakama zote
za Mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara.
Nae
mwenyekiti wa wanakusini forum (SEDO) Brigedia jeneral msaafu Aloyce Mwanjile
pamoja na kutoa pole aliupongeza uongozi wa Mkoa huo kwa namna
walivyoshughulika na maafa hayo pamoja na kuwaokoa wananchi.
Akipokea
misaada hiyo Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi aliwashukuru wadau hao kwa misaada
waliyoitoa kwa ajili ya waathirika huku akiwatoa hofu kuwa misaada hiyo ipo
katika mikono salama na itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment