Meneja wa Bank ya NMB kanda ya kusini Bi,
Janeth Shango kulia akikabidhi Meza na Viti kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mkoani
humo Shaibu Ndemanga jana katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mnolela
Halmashauri ya Mtama.
..................................................
NA
HADIJA HASSAN, LINDI
BANK
ya NMB yatoa Msaada wa Meza, Viti , Mabati pamoja na Kofia zake kwa Shule za
Sekondari za Wilaya ya Lindi Mkoani humo vyote vikiwa na thamani ya Shilingi
Mlioni 20.
Msaada
huo ni Meza150, Viti 150, Bati136 pamoja na kofia zake 26 ambazo zitagawiwa kwa
Shule Nne za Sekondari za Wilaya hiyo.
Msaada
huo umekabidhiwa na Meneja wa kanda wa Bank hiyo Janeth Shango kwa Mkuu wa
Wilaya hiyo Shaibu Ndemanga jana katika viwanja vya shule ya Sekondari Mnolela
Halmashauri ya Mtama.
Miongoni
mwa shule zilizonufaika na mgao huo ni pamoja na shule ya Sekondari Ng’apa,
iliyopo Manispaa ya Lindi ambayo imepatiwa viti 50 na meza 50, shule ya
Sekondari kitomanga Halmashauri ya Mtama meza 50 na viti 50, Mnolela Sekondari
halmashauri ya Mtama viti 50 na meza 50 pamoja na Shule ya Sekondari Kiwalala
Mtama ambayo imepatiwa mabati 136 pamoja na kofia zake 26.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi msaada huo Meneja wa NMB Benk kanda ya kusini Janeth Shango
alisema kuwa hatua ya Bank yao kutoa msaada huo ni kutaka kuunga jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya nne ya kuboresha sekta ya Elimu hapa
Nchini.
Shango
alisema kuwa kwa NMB changamoto za sekta ya Elimu na Afya Hapa Tanzania ni
jambo la kipaumbele kutokana na umuhimu wa sekta hizo kuwa ndio nguzo kuu ya
maendeleo kwa Taifa.
“sisi
kama NMB tumekuwa msitari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la
kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii ,ambapo kwa zaidi ya miaka saba
mfululizo tumeweza kuchangia 1% ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa
jamii inayotuzunguka” alisema Shango.
Hata
hivyo shango aliongeza kuwa mwaka 2020 Benk yao imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni
1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na
Afya . Kwa upande wake Rahma Athumani mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ng’apa
aliishukuru Bank ya NMB kwa kuwatatulia changamoto iliyokuwa inawakabili
Shuleni hapo ya Meza na Viti.
Alisema
kuwa kwa Darasa lao walikuwa wanalazimika kutumia Maabara kama Darasa kutokana
na changamoto hiyo ya meza na viti jambo ambalo lilikuwa linawaletea usumbufu
pale ambapo madarasa mengine wakitaka kujifunza kwa vitendo.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga aliishukuru
Bank hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika
kuboresha Sekta ya Elimu.
Ndemanga
alisema kuwa uboreshwaji wa vifaa vya kujifunzia pamoja na mazingira wezeshi ya
kufundishia ni miongoni mwa mpango mkakati kuinua ubora wa Elimu katika Mikoa
huo wa Lindi hivyo sehemu ya Meza na Viti ni hatua moja wapo ya kutekeleza
mpango huo mkakati.
Hata
hivyo Ndemanga aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na
Bank hivyo katika shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na majanga
yanapotokea huku akitoa wito kwa Taasisi zingine kuendelea kuunga mkono
jitihada hizo.
Meneja
wa Bank ya NMB kanda ya kusini Bi, Janeth Shango kulia akikabidhi Mabati Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Mkoani humo Shaibu Ndemanga jana katika viwanja vya Shule ya
Sekondari Mnolela Halmashauri ya Mtama.
No comments:
Post a Comment