Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa (kati
kati) akizungumza na wananchi wa kata ya Nianjema hawapo pichani katika mkutano
wa hadhara ambao aliuandaa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za
wananchi hao.
...............................................
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO.
BAADHI ya wazee wanaoishi katika kaya
masikini na mazingira magumu Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameiomba
serikali ya awamu ya tano kuingilia kati sakata la kero yao kubwa ya kuonewa
kwa kipindi kirefu kutokana na kutopatiwa fedha ambazo zinatolewa na
mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa ajili ya kujikimu kimaisha pamoja na
kuanzisha miradi midogo midogo.
Hayo yalibainisha wakati wa mkutano
wa hadhara ambao umeandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Zainabu Kawawa
kwa wananachi wa Kata ya Nianjema kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto
mbali mbali zinazowakabili ili kuzitafuatia ufumbuzi pamoja na kuweka mikakati
ya kuleta maendeleo kwa wananchi kwa ushirikiano wa serikali na jamii kwa
ujumla.
Aidha mmoja wa wazee hao akizungumza
kwa niaba ya wezake wanaoishi katika kaya masikini Ole Shamba alisema
kwamba wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika suala zima la upatikanaji wa
fedha kutoka TASAF hivyo wanajikuta maisha yao yanakuwa ni magumu kutokana na
kukosa mahitaji muhimu wao na familia zao.
“Kwa kweli huu mpango kiukweli
unatusumbua sana na leo hii kwa kuwa amekuja Mkuu wetu wa Wilaya Zainabu Kawawa
tumeona ni bora tuseme kilio chetu ambacho kimekuwa ni kero kubwa ya siku
nyingi maana hata sasa nimesahau kutokana na kipindi kimekuwa ni kirefu sana na
ukizingatia taratibu zote tumeshazikamilisha sasa nashindwa kuelewa kwa hiyo
tunaomba sana serikali yetu itusaidia katika suala hili,”aslisema Shamba.
Aidha katika hatua nyingine wazee hao
walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kuwa na utaratibu wa kufanya
mikutano na wananchi wake kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na
kumuomba alichukue suala hilo kwa uzito mkubwa ili fedha zote ambazo zinatolewa
ziweze kuwafikia walengwa na sio vinginevyo.
Kwa upande wake MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo
Zainabu Kawawa baada ya kusikiliza kilio hicho ameahidi kulivalia njuga suala
hilo na kuwaagiza watendaji wa TASAF kuhakikisha fedha zote zinazotolewa
zinawafikia walengwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa bila ya ubaguzi na
upendeleo na kuachana kabisa na vitendo vya kufanya ubadhilifu kwa maslahi yao binafsi
kwani atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia ,Mkuu huyo alibainisha kwamba
lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawaletea wananchi
maendeleo kupitia miradi mbali mbali na mifuko ambayo imeanzishwa hivyo
atahakikisha kwamba wale walengwa wote ambao wanaishi katika mazingira magumu
pamoja na kaya ambazo ni masikini wanawekwa katika utaratibu wa kusaidiwa
fedha kwa kuzingatai vigezo mbali mbali ambavyo vimetolewa na TASAF.
“Kwa kweli katika hili jambo mimi
nitalisimamia kweli kweli kwa kushirikiana na viongozi wangu wengine pamoja na
watendaji wa mamlaka husika lakini kikubwa fedha hizi ni lazima ziwafikie watu
ambao ni walengwa na wanaoishi katika kaya masikini, na kitu kingine watendaji
inabidi kuchunguza uhalisia wa kaya husika kama ni masikini au la na wananchi
msiwe wadanganyifu ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata haki zao, awe
bibi au babu sio anakaa Mkuranga unamwandikisha Bagamoyo hii hapana,”alisema Zainabu.
Kwa upande wake Mratibu wa
….TASAF Wilaya ya Bagamoyo Dionise Mahilane amesema kwamba kwa sasa wamejipanga
kuondokana na changamato ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi kuwa wadanganyifu
katika utoaji wa taarifa zao ili kuhakikisha inawasaidia wale ambao ni walengwa
na wanaishi katika kaya masikini kwa kuzingatia vigezo vilivyoweka sambamba na
kutoa elimu jumuishi kwa jamii.
Naye Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul
Pyalla alisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya
kaya masikini kutokupata fedha hizo watafanya zoezi la kupita katika mitaa ili
kutoa elimu ya watu ambao wanastahili kusaidiwa sambamba na kuhakiki orodha ya
kaya ambazo zinatakiwa kupatiwa msaada lengo ikiwa ni kuondokana na kero
hiyo ambayo imekuwa ni usumbufu mkubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Kulia Zainabu Kawawa
akiwa anasikiliza moja na hoja ambazo zilikuwa zinatolewa na wananchi wa kata
ya Nia njewa wakati wa mkutano huo amabao ulifanyika katika viwanja vya shule
ya msingi nia njema.
Mkuu wa kituo cha Polisi Bagamoyo,
Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP) Michael Kakoshi licha ya kulinda hali ya
usalama katika eneo hilo la mkutano wa hadhara akiwa anasikiliza changamoto
mbali mbali ambazo zilikuwa zikitolewa na wananchi wa kata hiyo ya Nianjema.
Baadhi ya wazee wa Kata ya Nianjema Wilayani
Bagamoyo wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo wa
hadhara ambao ulihudhuriwa na wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na viongozi
wa serikalia na wakuu wa Idara.
Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul Pyalla
akizungumza jambo na wananchi katika Mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa na
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi kero zao ili
kuweza kuzitafutia ufumbufu. (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment