Saturday, February 1, 2020

ULINZI NA USALAMA WA MTOTO NI JUKUMU LA JAMII NZIMA



 
Devotha Ndunguru Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Songea akisisitiza jambo
 NA Joyce Joliga


Wanawake Mkoani Ruvuma wameshauriwa kuwa walinzi  namba moja kwa watoto wao wachanga  na wale wenye umri mdogo wa miaka 3-8 kwa  kujenga tabia ya kukagua nguo za ndani za watoto wao pamoja na kuwakagua mara kwa mara ilikujua kama wamefanyiwa vitendo vya ukatili.

Kwa mujibu wa  Ofisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Songea Devotha Ndunguru anasema matukio ya watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili ni mengi Songea  hivyo Suala la Ulinzi na Usalama wa Mtoto ni jukumu la jamii nzima ili kuhakikisha ustawi  wa mtoto ili aweze kukua akiwa mwenye afya njema,furaha , na Amani


Anasema,jamii hasa wazazi wanapaswa kujenga utamaduniwakuwa karibu nawatoto wao  na kujenga urafiki ili waweze kuwaeleza pindi wanapopatwa na matatizo , ambapo  wakina mama wajenge tabia yakukagua  nguo za watoto watabaini iwapo watakuta uchafu mwingi  na kuweza kutoa taarifa polisi .
 Devotha , Anasema inaumiza kuona baadhi ya akina mama wanawaficha watu ambao wanawafanyia vitendo hivyo watoto wao ili tu kuweza kuendeleza mahusiano yao ya kimapenzi bila kujali hatima ya watoto wao hivyo ameiomba jamii kuwa mlinzi namba moja wa watoto kwa kufichua vitendo hivyo ili kukomesha tabia hizo 
“Vitendo vya watoto kufanyiwa ukatili  ni vingi , Wapo baadhi ya wakinamama  wamekuwa wakificha vitendo viya ualawiti wanavyopfanyiwa watoto wao na Mabwana zao , niwasii muwe walinzi namba moja kwa watoto wenu achene kuendekeza tamaa za miili .
Afisa huyo ametoa mfano wa Mama mmoja jina limehifadhiwa mkazi wa Majengo Manispaa ya Songea ambaye mwanae wa miaka 8 alilawitiwa na hawara yake ambapo mtoto ameharibiwa vibaya sehemu za siri hali ambayo ilimfanya awe anaomba kuingiliwa ovyo hata wakati wa masomo alijikuta akishindwa kuhudhuria vipindi na kutoroka kwenda kuingiliwa na huyo hawara wa mama yake  na baadaye mtoto alimweleza mama yake mchezo ambao anafanyiwa lakini Mama alimtisha mtoto na kumkataza kumtaja kwa watu na kwamba akimsikia tena atamuua.
Anasema, kutokana na hali hiyo mtoto huyo alitoa taarifa kwa walimu ambapo wali mwita Baba yake mzazi na kumweleza kisha alitoa taarifa polisi na ustawi wa jamii walimchukua mtoto na kumwamishia kituo cha watoto Yatima cha
  Mchungaji mwema kilichopo Mji mwema ambapo mtoto alipatiwa matibabu na kufanyiwa vipimo vyote ikiwa ni pamoja na  kupewa ushauri nasaha na kwa sasa anaendelea kulelewa katika kituo hicho na tayari Mtuhumiwa amefunguliwa kesi .
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoani Ruvuma SP  Anna Tembo anawataka wanawake kuwalinda watoto ili waweze kutimiza ndoto zao kwa kutoa taarifa za vitendo viovu wanavyofanyiwa na kuacha tabia ya kuwalinda waharifu kwani hilo ni kosa la jinai.
Anasema, tarifa iliyotolewa na kitengo cha  Dawati la jinsia  mkoani Ruvuma inaonyesha kuwa Watoto 279 Walibakwa Mkoani humo katika kipindi cha Januari 2018 – Julai 2019  huku watoto 21 wakilawitiwa .

Anasema,taarifa ya makosa ya ukatili wa kijinsia  na watoto  mkoani Ruvuma kwa kipindi cha mwaka 2018  hadi julai 2019 SP Anna Tembo alisema, katika kipindi cha januari –Desemba 2018  makosa ya kubaka yalikuwa 159ambapo kesi 58 zipo chini ya upelelezi na 31 mahakamani  na walishinda kesi 26  huku 44 zilishindwaza kubakwa wakati kesi za kulawiti zilizoripotiwa ni 10 ambapo 3 zipo chini ya upelelezi, tatu  zipo mahakamani na mbili zilishinda na mbili zilishindwa .

Alifafanua zaidi kuwa  januari – julai 2019 kesi zilizoripotiwa ni 120 , ambazo zipo chini ya upelelezi ni 62 , na zilizopo mahakamani 32  walishinda kesi 9 na walishindwa kwesi 17 zakubakwa , ambapokesi za ulawiti ni 11 , kati ya hizo tatu zipo chini ya upelelezi, sita zipo mahakamani na mbili zilizoshindwa  hali ambayo inaonyesha kuwa bado zinahitajika jitihada zaidi kukomesha .

Aidha, amewataka wazazi kuacha kutelekeza familia zao kwani hicho nacho ni chanzo cha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto ambapo kwa kipindi cha Januari  2018- Julai 2019 jumla ya kesi  110 ziliripotiwa  katika kitengo hicho.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Songea  Devotha Ndunguru alisema, bado kuna tatizo kubwa la vitendo vya ukatili kwa watoto kwani baadhi wanabakwa na kulawitiwa na watu wao wa karibu ,wakiwemo ndugu , madaereva bodaboda wanaowapeleka shuleni na Majirani.
Anaitaka jamii itoe taarifa na kufichua waharifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua kwani vitendo hivyo vinawafanya watoto kuharibika na kushindwa kutimiza ndoto zao , ambapo tayari wameshaunda kamati ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA)  ngazi ya mtaa 95  ngazi ya kata 21 na moja ngazi ya wilaya ilikupata taarifa hizo.
Lengo la kuunda kamati hizo ni kutokomeza ukatili  dhidi ya wanawake na watoto ili watoto waweze kukua kwenye sehemu zenye ulinzi na salama na kuweza kuondokana ukatili wakati wa ukuaji wao.

Kwa upande wake Vicent Ndumbaro anasema elimu inahitajika zaidi kwa jamii ili weweze kusaidia kupinga vitendo hivyo kwani mwaka jana kuna mwanafunzi aliwalawiti wanafunzi wenzie 6 kwa kuwalaghai kwa kuwapa pipi pia , kuna mtu mzima ambaye alikuwa na tabia ya kuwashawishi watoto kwa kuwapa pipi kisha anawalazimisha wamnyonye sehemu zake za siri wakati akitambua kuwa anaugonjwa wa TB na tayari watu hao wameshachukuliwa hatua za sheria.
Naye Magreth Simon anawataka wanawake wenye tabia ya kuficha watu wanaowafanyia vitendo vya ukatili watoto wao  waache tabia hiyo ambapo ameiomba serikali kuwachukulia hatua watuhumiwa na wazazi ambao wanaficha taarifa hizo ili iwe fundisho.

No comments:

Post a Comment