Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya
kuwasili katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake
aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika
na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akiangalia moja ya darasa linalotumika kufundishia wanafunzi
katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni
lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma
zinazotolewa na Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni akikagua dawati katika moja ya darasa linalotumika
kufundishia wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake
aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze
kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni(kulia) baada ya kukagua moja ya
chumba vinavyotumika kutoa huduma ya malazi kwa wanafunzi
katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni
lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma
zinazotolewa na Jeshi la Polisi.
................................................
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameutaka uongozi wa Shule ya Polisi Tanzania
kuwafundisha ueledi wapelelezi ili kuweza kupunguza msongamano wa mahabusu na
kesi ambazo zinasababishwa na upelelezi usio na kiwango.
Masauni ameyasema hayo mkoani
Kilimanjaro wakati wa ziara ya kutembelea Shule ya Polisi Tanzania lengo ikiwa
kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma za Jeshi la
Polisi.
“Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli
alipokua akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria aligusia suala la
wapelelezi kuwa chanzo cha mlundikano wa mahabusu katika magereza yetu na mimi
hii leo nimetoka gereza la Arusha nimeongea na wafungwa na mahabusu nao
wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kupindishwa na mbaya zaidi wengine
wamehukumiwa vifungo kwa ajili ya upelelezi usio makini.
Ni tatizo kubwa
haiwezekani Rais huyu alalamike kila siku sasa maagizo ya serikali kwa chuo
hiki jitahidini kupika vizuri wapelelezi wenu vizuri,tumpumzishe Rais wetu ana
mambo mengi,timizeni tu wajibu wenu”amesema Masauni.
Akizungumza katika ziara hiyo Kaimu
Kamandanti Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar amesema wamechukua maelekezo ya
serikali na wanaahidi kuyafanyia kazi ili yaweze kuleta tija huku akitaja idadi
ya wanafunzi waliopo shuleni hapo wakisomea fani mbalimbali.
“Shule yetu kwa sasa ina wanafunzi
856 kati yao wanaume 725 na wanawake ni 131 ambao wako katika mafunzo
mbalimbali na wote wanaendelea vizuri na masomo” amesema Kamishna Msaidizi Omar
Katika ziara hiyo ya Naibu Waziri
Masauni alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo
sehemu za kulala,madarasa,uwanja wa paredi,vyumba vya komputa na ukarabati
bwalo la chakula.
No comments:
Post a Comment