Na mwandishi wetu
Chama cha wahasibu Tanzania (TAA)
kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
pamoja na chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) wameandaa wiki ya
uhasibu, hamira ikiwa kuwaleta karibu wahasibu na jamii.
Kwa miaka mingi wahasibu walikuwa wanakaa
nyuma ya kompya zao wakifanya kazi zao, hawakuweza kuwa karibu najamii,wengine
walionekana kuwa kikwazo cha kupata fedha zao, lakini wameamua kujitokeza
hadharani na kuwaambia watu kuwa wao sio kama wanavyowafikilia.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana, mwenyekiti wa chama chawaasibu Tanzania (TAA) alisema wafanyabiashara,
wajasiliamali, wafugaji, wavui na taasii mbalimbali watapata fursa ya kupata
ushauri.
Kwa mara ya kwanza wiki ya Uhasibu
itaadhimishwa kwa siku 6 kuanzia March 9 hadi March 14, Wiki ya Uhasibu
inafanyika kwa ajili ya kuifahamisha jamii umuhimu wa taalum ya uhasibu kwa
ajili ya uchumi wa viwanda na maendeleo ya jamii.
Hii itakuwa inawaleta pamoja wadau
mbalimbali kushiriki na kutambua kazi ya Uhasibu na Wahasibu wanaofanya kazi
katika taasisi mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali za majukumu ya taaluma hiyo,
ambapo kutakuwa na huduma ya kushauri na kuwawezesha wahasibu kusonga
mbele kitaaluma.
Kwa Wahasibu ambao wana malengo ya
kufungua kampuni zao binafsi au taasisi zozote za Uhasibu hiyo itakuwa ni fursa
nzuri kwao kukutana na wenye makampuni wabobemzi na itakuwa ni fursa nzuri
kushea nao mawazo.
No comments:
Post a Comment