Mwenyekiti
wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi akikabidhi msaada kwa
waathirika wa mafuriko eneo la Njinjo wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi, akiwa na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Musa Buluki, pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi ya hiyo wakiwasili eneo la Njinjo wilayani Kilwa kwaajili kugawa misaada kwa wananchi walioathirika na mafuriko kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Akizungumza katika zoezi hilo, Aref alisema anawashukuru wananchi wote kwa ujumla walioungana na The Islamic Foundatio kufanikisha misaada hiyo ili kuwasaidia watanzania waliokumbwa na mafuriko.
Alisema taasisi hiyo iliweka makadirio ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 100 lakini kwa muitikio ulivyokuwa mkubwa makusanyo ya michango imefika zaidi ya milioni 110.
Aidha, alisema wanatekeleza hayo kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu yanayotaka kusaidiana katika matatizo bila ya kujali dini, rangi, wala kabila.
Vijana
wakujitolea wakiwa katika harakati za kugawa misaada iliyokusanywa na The
Islamic Foundation kwa waathirika wa mafuriko huko Njinjo wilayani Kilwa.
Sehemu ya wananchi walioathirika na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini, wakisubiri utaratibu wa kugaiwa misaada hiyo kutoka kwa taasisi ya The Islamic Foundation ambayo makao yake makuu ni mkoani Morogoro.
Sehemu ya misaada hiyo ikiwa imepangwa kwa utaratibu wa kugawa kwa wahusika.
No comments:
Post a Comment