NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Vitambulisho
vya wajasiriamali (machinga) vyapandisha huduma za mikopo zinazotolewa na
shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Lindi kwa zaidi ya
asilimia 124%.
Ongezeko
hilo la kiwango cha pesa zilizokopeshwa kwa wajasiriamali limepanda kutoka
shilingi ML.79 Desemba mwaka 2015 mpaka kufikia shilingi ML.224 Desemba mwaka
2019.
Hayo
yameelezwa na meneja wa Shirika hilo jana Mwita Kasisi alipokuwa akitoa taarifa
ya huduma za mikopo katika khafla ya utowaji wa mafunzo ya ujasiriamali na
usimamizi wa mikopo kwa wajasiriamali.
Kasisi
alisema miongoni mwa sababu zilizofanya huduma hizo za mikopo kwa wajasiriamali
na wafanya biashara wa kati wa mkoa huo ni kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa
na serikali kwa wajasiriamali hasa ya kutoa vitambulisho.
Alisema
tokea vitambulisho hivyo vimeanza kutolewa shirika limeweza kuwatambua kwa
urahisi wajasiriamali ambao wanakidhi vigezo vya kupatiwa mikopo.
Kasisi
alieleza sababu nyingine ya upandaji huo wa huduma za mikopo ni uwelewa wa
kutosha walionao wajasiriamali kupitia Elimu mbali mbli inayotolewa na shirika
hilo juu ya faida za mikopo katika kukuza na kueneleza biashara zao.
Kasisi
alisema kuwa ongezeko hilo pia limepanda kwa wastani wa uchukuwaji wa mikopo
kwa mtu mmoja mmoja kutoka wastani wa milioni 1 kwa kila mjasiriamali mpaka wastani
wa milioni 2.1 kwa mjasiriamali mmoja kwa mwaka.
Kasisi
aliongeza kuwa kwa kipindi hicho cha miaka minne jumala ya pesa shilingi
milioni 895.9 zimetolewa kwa wajasiliamali 414 kwa wastani wa shilingi milioni
2.1 kwa kila mjasiliamali mmoja.
Akifungua
mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga aliwataka wajasiliamali
hao kuyatumia mafunzo hayo kwa kuonyesha mabadiliko katika shughuli zao kwa
kujitofautisha kati yao na wafanya biashara.
"Lengo
la kuwaweka hapa tofauti na kuwapatia mikopo lakini pia mnafundishwa
kuziongezea thamani bidhaa zenu, uwezi kununua magauni na vitenge kariakoo
ukaja kuuza Lindi ukajiita wewe ni mjasiliamali tunatamani baada ya mafunzo
haya tuone tofauti katika shughuli zenu kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo
" alisisitiza Ndemanga.
Ndemanga
pia alisisitiza nidhamu ya fedha za mikopo walizokopeshwa wajasiliamai hao
kutumia kwa malengo waliyokusudia ili waweze kurejesha kwa wakati.
Kwa
upande wake Amina Khalphani Mjasiliamali Manispaa ya Lindi Mkoani humo
aliishukuru Serikali kupitia Shirika hilo la SIDO kwa kuwawezesha kuwapa
mafunzo ya ujasiliamali na usimamizi wa mikopo itakayowawezesha kukuza na
kuendelezabiasharazao.
No comments:
Post a Comment