NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
WANANCHI
Mkoani Lindi wametakiwa kuitumia wiki ya sheria kupata Elimu mbali mbali
inayohusiana na mambo ya Sheria na haki zao kupitia vituo mbali mbali
vilivyotengwa na mahakama kwa ajili ya kutoa elimu.
Wito
huo umetolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Mkoa wa Lindi Elimo
Masawe kwenye ufunguzi wa wiki ya Sheria uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
viwanja vya mahakama ya mkoani humo.
Wiki
hiyo ya sheria huanza february 1 na kuhitimishwa february 6 kila mwaka ikiwa ni
ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli za mahakama hapa nchini ambapo kwa mwaka
huu 2020 Kauli mbiu ya wiki ya sheria ni “uwekezaji na biashara wajibu wa
mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji”
Masawe
alisema katika Mkoa wa Lindi na wilaya zake kwa ujula imetenga vituo zaidi ya
50 kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya sheria Alisema elimu
hiyo ya kisheria itatolewa kwa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama kama
vile, jeshi la polisi, magereza, mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Shirika la
kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) pamoja na wadau wengine.
Akielezea
vituo vya kutolea elimu, alisema kuwa vituo hivyo vimewekwa katika maeneo yenye
misongamano wa watu kama vile masoko makubwa na madogo, vituo vya mabasi pamoja
na kutoa elimu katika shule za msingi na sekondari, makundi ya wajasiriamali
wadogo na wakati, wafanya Biashara ,vyuo vya ufundi pamoja na makundi ya
madereva bajaji na boda boda.
“Lengo
kubwa la kutaka kufikia makundi haya yote tunataka jamii ituelewe sana kwa
sababu jamii ikishatuelewa itakuwa na nafasi ya ujasiri wa kusimamia haki zao
kwani kitendo cha mtu kuijua haki yake ni sawa na kuongeza ujasiri wa maisha”
Nae
mwenyekiti wa kamati ya elimu , Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya
Lindi, Maria Batulaine alisema kuwa miongoni mwa mambo watakayowafundisha
wananchi kwenye vituo hivyo kuhusiana na sheria ni pamoja na kujua sheria za
jinai na madai, kuwajulisha shughuli zinazofanywa na mahakama, huduma
zinazotolewa na mahakama na mambo mbali mbali ya kisheria.
Akizindua
wiki hiyo ya sheria katibu tawala wa wilaya ya Lindi Tomas Safari kwa niaba ya
Mkuu wa Wilaya Hiyo Shaibu Ndemanga, aliwataka wadau wa mahakama kudumisha
mshikamano ili kuhakikisha haki ya mwananchi inapatikana kwa wakati.
No comments:
Post a Comment