Kijana mmoja (jina linahifadhiwa) (10) ambae ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi
hotel tatu wilayani Kilwa akiwa amebeba beseni la majani ya kunde na kunde kwa
ajili ya kupeleka sokoni tayari kwa kuuza.
Kijana mmoja (jina linahifadhiwa) (10) ambae ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi
hotel tatu wilayani Kilwa akihojiwa na mwandishi wa BAGAMOYO KWANZA BLOG kijijini hapo huku akiwa ameandaa beseni la majani ya kunde na kunde kwa
ajili ya kupeleka sokoni tayari kwa kuuza, Picha zote Na Hadija Hassan.
........................................................
NA
HADIJA HASSAN, LINDI
BAADHI
ya watoto waliochini ya miaka 18 wanaoishi katika kata ya hotel tatu wilayani
kilwa Mkoani Lindi hutumika kufanya biashara ndogo ndogo za ujasiriamali ili
kuongeza pato la familia.
Hayo
yamebainika baada ya BAGAMOYO KWANZA BLOG kufika kijijini hapo na kukuta baadhi
ya watoto wenye umri wa kwenda shule wakijihusisha na biashara hizo ambapo
wamedai kuwa wamelazimika kufanya hivyo ili kuweza kupata fedha ya kupata
chakula BAGAMOYO KWANZA BLOG ilimshuhudia kijana mmoja (jina linahifadhiwa) (10) ambae ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi
hotel tatu wilayani Kilwa akiwa amebeba beseni la majani ya kunde na kunde kwa
ajili ya kupeleka sokoni tayari kwa kuuza.
Mtoto
huyo alisema kuwa hiyo ni kawaida kwa mama yake kumpatia biashara ndogo ndogo
kwa wakati tofauti kwenda kutembeza mitaani ama kuuza sokoni kwa ajili ya
kujipatia pesa ya kuendeshea maisha yao.
“hizi
kunde kanipatia mama nikauze kwa kutembeza mtaani lakini siki nyingine mama
huwa anapika keki au maandazi ambayo naendaga kuuza sokoni , pale tunakuwaga watoto
wengine kila mtu akiwa na biashara yake ambao tunakujaga kuuza vitu mbali
mbali” alieleza mtoto huyo.
Kwa
upande wake mama mzazi wa mtoto huyo alikiri kumtumia mtoto wake katika
biashara ndogo ndogo huku akieleza kuwa analazimika kufanya hivyo kutokana na
hali ngumu ya maisha
“huyu
ana wiki sasa hajaenda shuleni anahali ya homa na yupo kwenye dozi, hata hizo
kunde mlizomkuta nazo kwa leo sikumtuma kwenda kuuza ila kwa sababu njaa
inawauma na hapa ndani hakuna chakula baada ya mimi kufika na hizi kunde kutoka
shambani yeye akaona bora akaziuze ili tupate angalau pesa ya kununua anga”
Nae
mtendaji wa kijiji cha hotel tatu Abdalah Shante amekiri kuwepo kwa baadhi ya
watoto katika kata hiyo kutumikishwa na wazazi ama walezi wao katika kufanya
biashara ndogo ndogo ambapo alisema kuwa hali hiyo inatokana na hali ngumu ya
kipato walionao wazazi hao.
“Wakazi
wa kata hii vipato vyao ni vidogo hivyo wanategemea biashara ndogondogo kama
vile maandazi, vitumbua, kashata na vitu vingine vidogo vidogo kama hivyo, kwa
hivyo baada ya muda wa masomo wazazi huwapatia watoto wao biashara hizo wenyewe
wakiwa shambani ili watakaporudi kutoka huko waweze kununua unga ua mboga
wanakula” alieleza Shante.
Licha
ya kukiri kufahamu kuwa sheria hairuhusu kuwatumikisha watoto Shante alisema
kwamba kutokana na hali halisi ya maisha wao kama serikali ya kijiji jitihada
walizozichukuwa za haraka ni kuzungumza na wazazi wa watoto ambao wanajihusisha
katika biashara kuwaeleza licha ya kuwatumia watoto hao kwenye biashara zao
lakini wahakikishe watoto hao wanahudhuria shuleni bila kukosa
“kutokana
na hali ya maisha ilivyo tumeona hata tukiwakataza wasiwatumie kabisa watoto
hao kama vile tutawaonea tu bure kwa maana biashara hizo ndizo zinazowapatia
chakula baada muda wa shamba ila tulichowaambia wahakikishe hao watoto wao
wanafanya hizo biashara baada ya muda wa shule kupita ili watoto hao wasikose
masomo kutokana na biashara hizo” aliongeza.
No comments:
Post a Comment