NA
MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
HALMASHAURI
Ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto katika
shughuli za ugani ikiwemo usafiri wa uhakika kuwafikia wakulima ambao wapo
vijijini na vitongoji.
Aidha
kuna vijiji 31 ambavyo havina maofisa, hivyo kutokana na changamoto hizo
wakulima wamekuwa hawapati huduma yenye tija kwa kushindwa kufikiwa na maafisa
ugani mara kwa mara.
Changamoto
hizo zimewekwa bayana na mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze, Bi Amina
Kiwanuka katika makabidhiano ya pikipiki kumi zenye thamani ya mil.25 kwa
maofisa ugani wa vijijini na magari ya halmashauri mapya mawili yenye thamani
ya zaidi ya milioni 290.
Alieleza,
kutokana na changamoto hiyo kupitia idara ya kilimo halmashauri ya Chalinze
imejiwekea malengo hadi kufikia 2021/2022 iweze kununua pikipiki 50 kutoka
kwenye bajeti za mapato ya ndani kwa ajili ya maofisa ugani wa vijiji na kata.
“Pikipiki
hizi zitawasaidia maofisa ugani hawa kuwatembelea wakulima kwa wakati na kuwapa
huduma ambazo zitawawezesha kuongeza tija katika sekta ya kilimo”alifafanua
Amina.
Hata
hivyo Amina alielezea, maofisa hao wataweza kutumia pikipiki hizo kwenda
kuhudumia katika vijiji ambavyo havina maofisa ugani.
Nae
mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu alieleza, halmashauri
hiyo ilianza kutenga bajeti ya pikipiki mwaka wa fedha 2018/2019 na kununua
pikipiki 15 zenye thamani ya milioni 37.5 na kupewa maofisa ugani wa kata.
“2019/2020
zimenunuliwa pikipiki hizi kumi za milioni .25 na kupewa maofisa ugani wa
vijiji vya pembezoni pia tumetenga milioni 32.4 kwa ajili ya pikipiki 12 kwa
mwaka 2020/2021″
Zikatimu
alisema ,kutokana na umuhimu wa usafiri ili kurahisisha utendaji kazi
magari yaliyonunuliwa nayo yanakwenda kusaidia kusukuma kazi za idara
mbalimbali ambazo zinahitaji matokeo kupitia usafiri.
Kwa
upande wake ofisa ugani wa kijiji cha Kimange, Aloyse Jumanne aliishukuru halmashauri
kwa kuiona changamoto ya ukosefu wa usafiri na kuifanyia kazi.
Alibainisha
kuwa, usafiri huo unakwenda kujibu kero za wakulima ambao walikuwa hawafikiwi
kwa wakati na kujikuta wakishindwa kunufaika na kilimo cha kisasa.
No comments:
Post a Comment