Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Wilayani Bagamoyo, Saidi Zikatimu, kulia akizungumza na waandishi wa Habari, Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Edesi Lukoe.
Halmashauri ya Chalinze, Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, imetenga kiasi cha sh.mil 36 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Chalinze, Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, imetenga kiasi cha sh.mil 36 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri hiyo.
Kati ya fedha hiyo wenyeviti hao wanalipwa kila
mmoja sh.30,000 kwa mwezi hadi mwezi july mwaka huu
itakapokoma bajeti hiyo.
Akizungumzia kuhusiana na mpango huo,kwa waandishi
wa habari mjini hapo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu
,alisema halmashauri hiyo imeamua kuwalipa posho wenyeviti hao kwani
wanafanyakazi kubwa ndani ya miaka mitano bila kuambulia chochote.
Alisema wameshirikiana na mbunge wa jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Kikwete,kuona namna ya kuwatupia jicho wenyeviti hao wa
vijiji na vitongoji.
Aidha Zikatimu alieleza kwamba ,fedha hizo
zitawawezesha wenyeviti hao kujikimu na kuondokana na hali ya kuuza ardhi za
vijiji kwa visingizio vya kukosa posho ama mishahara.
Alibainisha ,fedha hiyo pia itaweza kuwasaidia
wenyeviti hao kuwa na morali na ari ya kuchapakazi kwenye maeneo yao na
wamejipanga kila mwaka watakuwa wakitenga fedha hizo.
“Kiasi hiki cha sh.mil.36 ni fedha watakazolipwa
hadi july 2017 na bajeti inayofuata tutaangalia kama kuna uwezekanao wa
kuongeza kiasi kilichopangwa katika bajeti hii ama ibakie kiasi kilichotengwa
kwenye bajeti hii”alifafanua Zikatimu.
Hata hivyo Zikatimu alisema ,wanachotarajia ni
wenyeviti hao kuendelea kuwa wasimamizi wazuri katika vyanzo vya mapato na
kuachana na tabia ya kuuza maeneo ya vijiji kinyume na taratibu.
Alisema wanawahamasisha kusimamia vyanzo vya mapato
ili kuinua makusanyo hasa ya vyanzo vya ndani ikiwemo vizuizi mbalimbali vya
pembezoni na ndani ya mji huo.
Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa halmashauri nyingine nchini kuwaangalia wenyeviti hao kwani kwa Chalinze imeshaleta tija ndani ya miezi sita tangu kuanza kwa mpango huo.
Aliiomba serikali na halmashauri hizo ziangalie
namna ya kuwatengea fedha wenyeviti wa vijiji na vitongoji kama ilivyo kwa
madiwani na wabunge wanavyotengewa posho wakimaliza muda wao,ili waweze kuwa na
moyo wa kufanya kazi pasipo kukosa chochote.
“Halmashauri ni sehemu ya kwanza na serikali kuu ni
sehemu ya pili,hivyo halmashauri zionyeshe nia ili serikali ilione hili,kwa
kuwapa kipaombele ya kuwatengea fedha bila kuwaacha”.
Zikatimu alisema wenyeviti hao wanasimamia chaguzi
mbalimbali na ilani ya CCM hivyo waangaliwe katika suala hilo ili waweze
kujiona ni viongozi wanaoaminika kwenye maeneo yao.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika moja ya vikao vya madiwani Halmashauri ya Chalinze.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakiwa katika moja ya vikao vya Baraza la madiwani Chalinze.
No comments:
Post a Comment