Thursday, January 5, 2017

SERIKALI YAWEKA MPANGO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikianana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini, (VETA) wanaendesha mpango wa Kutathmini na Kurasimisha Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo.

Katika mpango huu una fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi wako, kupewa mafunzo kuziba mapungufu, kisha kutunukiwa cheti.

Fani zitakazohusika ni: UASHI, USEREMALA, UFUNDI MAGARI-MAKENIKA, UPISHI, UHUDUMU WA HOTELI, BAR NA MIGAHAWA.

Ikiwa unakidhi masharti yaliyotajwa, fika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya iliyoko karibu uchukue na kujaza fomu za maombi bila malipo. Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 05 hadi 25 Januari, 2017.

Watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa ajili ya usaili kuanzia tarehe 10 Februari 2017.

Mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi, wasiliana na Mratibu wa Programu (VETA) hii kwa namba 0715 55 55 85.

IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU

4/01/2017

No comments:

Post a Comment