Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela,
Mwenye fulana ya Orange katikati, akiongoza mazoezi ya viungo pamoja na wafanyakazi wa Halmashauri ya Bagamoyo leo jumamosi 28
january 2017, katika uwanja wa Mwanamakuka
mjini Bagamoyo, Kulia ni Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja,
Iddi Musira, na Kushoto ni Kamanda wa
TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo, Raymond Katima.
Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela,
Mwenye fulana ya Orange, katikati, akiongoza mazoezi ya kukimbia pamoja na watumishi
wa Halmashauri ya Bagamoyo leo jumamosi 28 january 2017, wa kwanza kulia mwenye fulana nyekundu ni Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo, Raymond Katima, wa pili kulia mweye Tracksuit, ni Mkuu wa Gereza
la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza- Muyengi Bulilo na wakwanza kushoto ni Mkuu
wa kituo cha Polisi Bagamoyo, Mrakibu wa
Polisi, SP- Ngonyani.
Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela
akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi leo Tarehe 28 January 2017 katika
Uwanja wa Mwanamakuka Bagamoyo mjini.
....................................
Wananchi wilayani Bagamoyo wametakiwa kujenga
Tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara
ili kujenga afya za miili yao.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanyika kwa
mazoezi katika uwanja wa mwanamakuka Bagamoyo mjini, kati bu Tawala wa wilaya
ya Bagamoyo Erica Yegela alisema hali hiyo itasaidia kuondoa magonjwa
mbalimbali ambayo yanasababishwa na kuwa na mafuta mengi mwilini.
Kwa upande wake Afisa Michezo wilaya ya Bagamoyo,
Vedastus Mziba, alisema mazoezi hayo yamefanyika kwa ufanisi na kwamba kipimo
umbali waliotem bea umelingana na afya za washiriki ambapo imesaidia
kuchangamsha miili ya watu.
Nae Afisa utamaduni wilaya ya Bagamoyo, Hamisi
Kimenya alisema wanapaswa kufanyamazoezi kila wakati badalaya kusubiri kuambiwa
na viongozi.
Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela
alisema jumamosi ya katikati ya mwezi itakuwa ni siku yausafi na mazoezi ambapo
alisema yataanza mazoezi katika Uwanja wa Mwanamakuka, na baadae kuelekea
sehemu ya kufanya usafi.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo
ya usafi na mazoezi ili kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli ya kufanya usafi na agizo la Makamo
wa Rais, Samia Suluhu la kufanya mazoezi
ili kuepuka magonjwa mbalimbali.
Mazoezi hayo yaliyofanyika leo katika wilaya ya
Bagamoyo yametanguliwa na usafi ambapo awali ulifanyika usafi katika ofisi ya mkuu wa wilaya.
Mazoezi hayo pamoja usafi vimefanyika na taasisi
mbalimbali za serikali ikiwemo, Jeshi
la Polisi, Askari Magereza, TAKUKURU,
Vyuo vya Ukutubi na Tasuba Jeshila akiba na wakufunzi wake, pamoja na
watumishi kutoka idara mbalimbali za Halmashauri ya Bagamoyo.
Mazoezi na Usafi vimeongozwa na Katibu
Tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela akiwa na mkuu wa Gereza la Kigongoni,
Mrakibu wa Magereza, Muyengi Bulilo, muwakilishi wa
OCD Bagamoyo, Mrakibu wa Polisi
SP. Ngonyani, Pamoja na Madiwani.
Mkuu wa kituo cha Polisi Bagamoyo, Mrakibu wa
Polisi, SP- Ngonayni, akiongoza Askari polisi kufanya Usafi kwenye Ofisi ya Mkuu wa iwlaya ya Bagamoyo, leo Tarehe 28
January 2017.
Askari wa
kikosi cha zimamoto Bagamoyo wakishiriki usafi katika ofisi ya mkuu wa wilaya
ya Bagamoyo, kabla ya kufanya mazoezi ya viungo.
Wananchi mbalimbali wakiwa katikaOfisi ya mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, wakishiriki usafi
kabla ya kuelekea kwenye mazoezi ya viungo.
Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela,
wa kwanza kushoto, Mkuu wa Gereza
la Kigongoni, Mrakibu wa magereza-
Muyengi Bulilo, katikati na Mkuu wa kituo cha Polisi Bagamoyo, Mrkibu wa
Polisi, SP- Ngonyani, kwanza kulia wakiandaa kuondoka Ofisi ya
mkuu wa wilaya kuelekea kwenye
mazoezi ya viungo.
Askari Polisi,
Magereza, Uhamiaji , Zimamoto, Watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya
Bagamoyo na wananchi wengine wakiwa
kwenye Mstari tayari kwa kuondoka kuelekea kwenye mazoezi ya viungo.
Safari ya kuelekea kwenye uwanja wa mwanamakuka,
ilianza kwenye Ofisi ya mkuu wa wilaya Bagamoyo, kupitia uwanja wa
Majengo, Stendi ya Kongoe,
Mwembe mkavu, Barabara
mpya ukuni, Kosovo na kutokea uwanja wa Mwanakalenge.
Vijana wa
Soba House Bagamoyo, nao hawakubaki nyuma kwenye mbio hizo kuelekea uwanja wa
mazoezi, wakiongozwa na Meneja wa kituo hicho Godwin Msilu, (Mjeda). anaesikiliza simu, kulia.
Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela,
Mwenye fulana ya Orange katikati, akiongoza mazoezi ya viungo pamoja na wafanyakazi wa Halmashauri ya Bagamoyo leo jumamosi 28
january 2017, katika uwanja wa Mwanamakuka
mjini Bagamoyo, Kulia ni Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja,
Iddi Musira, na Kushoto ni Kamanda wa
TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo, Raymond Katima.
Bagamoyo Jogi , nao walikuwa mstari wa mbele
katika mazoezi ya viungo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji mdogo wa
Bagamoyo, Athumani Stili, wa kwanza
kulia akiwa kwenye mazoezi ya viungo leo.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Bagamoyo, Mrakibu wa
Polisi, SP-Ngonyani akiwa kwenye mazoezi ya viungo leo katika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini, anaefuata ni mkuu wa Gereza
la Kigongoni, Mrakibu Magereza,
Muyengi Bulilo.
No comments:
Post a Comment