Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy.
......................................
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Bagamoyo imepitisha Bajeti ya bilioni 41
kwa mwaka wa fedha 2017/18 ikiwa na
ongezeko la aslilimia 14 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2016/17.
Awali
akiwasilisha Bajeti hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Bagamoy,
Malboard Kapinga amesema malengo ya bajeti hiyo ni mapato kutoka makusanyo ya ndani, Ruzuku kutoka
Serikali kuu pamoja na wahisani
mbalimbali.
Baada ya
kuwasilishwa kwa Bajeti hiyo
wajumbe wa kikao hicho wamepitia bajeti hiyo ukurasa kwa ukurasa na
hatimae kujiridhisha na kuipitisha Bajeti hiyo ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Bagamoyo, Aliy Aliy, amesema Baraza hilo limeridhia Bajeti hiyo.
Mwenyekiti huyo
wa Halmashauri ya Bagamoyo, amesema Bajeti hiyo ya Bilioni 41 inawalenga
wananchi wa Bagamoyo na kwamba kazi
kubwa ya madiwani ni
kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha zinakwenda kwenye
utekelezaji wa miradi ya maendeleo
No comments:
Post a Comment