Monday, January 9, 2017

MGUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AGAWA VITABU VYA KUJIFUNZIA MASHULENI.

97
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini,Hamoud Jumaa,mwenye kibaghalashia,akikabidhi kontena la vitabu vya kujifunzia katika shule za msingi na sekondari ,zaidi ya 40,000 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Tatu Selemani,wa pili kulia,(Picha na Mwamvua Mwinyi)
 10

Mbunge wa Kibaha Vijijini,Hamoud Jumaa,akizungumza jambo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu mbalimbali katika shule za msingi na sekondari,katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
 ........................

Na Mwamvua Mwinyi-Kibaha.

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha vijijni ,Hamoud Jumaa ametoa kontena la vitabu vya kujifunzia katika shule za msingi na sekondari za halmashauri ya wilaya ya Kibaha vilivyogharimu zaidi ya sh.mil. 66.

Vitabu hivyo vipo zaidi ya 40,000 ikiwemo vya masomo ya sayansi,hisabati na lugha ambavyo vitagawanywa katika shule za msingi 37 na sekondari 8 zilizopo katika halmashauri hiyo.

Akikabidhi msaada huo ,kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Tatu Selemani na mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Mansoor Kisebengo,kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani,Jumaa aliomba vitabu hivyo vitunzwe na kusimamiwa.

Alieleza ,ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni waakti wa ziara yake jimboni hapo na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.

“Namuunga mkono rais katika harakati zake za kutatua kero mbalimbali za kielimu ikiwemo kutoa vitabu kwa shule za msingi na sekondari ili wanafunzi wajenge tabia ya kupenda kusoma” alisema Jumaa.

Jumaa anatoa vitabu hivyo ikiwa sasa ni awamu ya tatu ambapo awamu mbili zilizopita alitoa mwezi agost mwaka 2016 vitabu vyenye thamani ya mil.99.

Hata hivyo ,mbunge huyo alieleza kwamba wameshajenga maktaba 24 , lakini tatizo kubwa lililo mbele yao ni upungufu wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu na matundu ya vyoo.

Alifafanua,halmashauri ya wilaya ya Kibaha ina kata 14 na shule za msingi 37 na jumla ya wanafunzi ni 6,414 na tayari shule zote za msingi zimepata madawati kupitia michango ya wadau, vyanzo vingine vya mapato ya halmashauri na kutoka ofisi ya bunge.

Jumaa alisema ataendelea kusimamia kero zinazokabili jimbo hilo katika sekta mbalimbali kwa awamu kulingana na uwezo alionao .

Akipokea msaada huo,mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Tatu Selemani,alisema kimsingi vitabu hivyo vitaongeza maarifa licha ya kutoka nje ya nchi (Marekani),kwani vipo vinavyoendana na mitaala ya  nchini Tanzania.

Alisema hali ya upatikanaji wa vitabu bado lakini kutokana na  serikali kuu inaratibu kupitia ofisi ya rais tamisemi ndio inaonunua na kupelekea kwa awamu  katika maeneo mbalimbali anaimani tatizo hilo litakwisha .

Nae mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambae pia ni diwani wa Kwala ,Mansoor Kisebengo,alishukuru na kusisitiza kuwa mazingira mazuri ya kujifunzia humfanya mwanafunzi aweze kuwa msikivu darasani .

Kwa niaba ya chama cha wananchi (CUF)katibu mstaafu wa chama hicho,Kibaha Vijijini,Mwinjuma Matulanga,alimpongeza mbunge Jumaa na serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ilani ya CCM katika sekta ya elimu.
12
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Mansoor Kisebengo, akizungumza jambo wakati wa makabidhiano ya msaada wa vitabu mbalimbali katika shule za msingi na sekondari uliotolewa na mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
 13


Kontena la futi nne,lililoletwa na mbunge wa Kibaha Vijijini,Hamoud Jumaa, ambalo  limebeba vitabu mbalimbali vya ziada ambavyo vitatumika kujifunzia katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha .


No comments:

Post a Comment