Friday, January 13, 2017

TIF YAGAWA SADAKA YA NYAMA YA MILIONI ZAIDI YA 200.


Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake makuu  mjini  Morogoro, imegawa   sadaka ya nyama kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na  Morogoro ikiwa ni sehemu ya utekelezaji  wa majukumu ya utoaji  wa sadaka.
Akizungumza wakati wa zoezi  ililo jijini Dar es Salaam, Katibu  Mkuu  wa TIF  Ally Ally Ajirani, alisema Nyama hiyo imepokelewa  kutoka nchini   Saudi Arabia ikiwa ni sadaka inayotolewa kila mwaka ambapo mwaka huu TIF imepokea Kontena mbili  na kuzigawa  kama  ilivyokusudiwa.

Alisema TIF  imebeba gharama  zote za kuipokea nyama hizo hapa nchini  ikiwa na  lengo  la  kutimiza  kile kilichokusudiwa  ambacho ni kuzigawa kwa wahusika,  na kuongeza kuwa, nyama hizo ambazo  ni katoni  2,465 thamani yake ni  shilingi milioni 239, 850,000.

 Alisema katika sheria  ya  uislamu sadaka hutolewa kwa  watu wote, na kwamba  Taasisi ya  The  Isalamic  Foundation mara kadhaa imekuwa ikigawa misada kwa  watu  mbalimbali  bila ya  kujali  dini  zao  lengo  likiwa  ni kuwafikia  watu  wenye  mahitaji.

Alifafanua  kuwa,  vipo  vitu vitu vinavyowahusu  waislamu tu  huku  akitolea mfano wa  zaka  ambayo inatakiwa kupewa watu  maalum kwa mujibu wa  mafundisho yaliyomo ndani ya Qur ani.

Akizungumzia  kufanikiwa kwa  TIF  katika  kugawa  misada  mbalimbali, Ajirani,  alisema hiyo ni kutokana  na viongozi wake  hufanya  kazi kwa uadilifu,  uaminifu,  ukweli  na uwazi hali inayopelekea wahisani  mbalimbali kuendelea kuiamini  TIF  na  kufikisha  vitu  mbalimbali kwaajili ya  kusimamia ugawaji  wake.

Wakizungumza mara  baada ya kupkoea msaada huo  waislamu na wakazi wa jiji   la  Dar  es Salaam walisema kuwa wanaipongeza  Taasisi ya The  Islamic  Foundation  kwa kusimamia  vyema matukiombalimbali ya ugawaji  wasadaka  ikiwemo nyama hiyo ambayo  wameipata bila ya bughudha yoyote.

Aidha, waliwaomba viongozi  wa TIF  kuwa na  moyo wa subira  katika kutekeleza majukumu yao  ili  waislamu  na  wasiokuwa waislamu  waweze  kufaidika  na  huduma  zinazotolewana  TIF.

Walisema misaada kama hiyo iwe  endelevu ili waislamu  wapate kujua umuhimu wa kuwepo Taasisi hiyo ya TIF.
                                                           
Kwaupande wake Naibu  katibu   Mkuu wa The  Islamic Foundation, Musa Buluki ambae  alisimamia ugawaji  wa nyama  katika  mji  wa Mkoani  Morogoro, alisema  TIF  inajali  makundi  ya  watu mbalimbali katika jamii na hivyo  kufikisha  msaada katika maeneo  na watu  wenye  uhitaji.









No comments:

Post a Comment