Msafara
wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akiwa na
mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano leo mara baada ya kuwasili Ikulu.
mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano leo mara baada ya kuwasili Ikulu.
Msafara
wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan ukiwasili katika viwanja vya Ikulu
leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo
katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es salaam , Rais huyo yuko nchini kwa
ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais
wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerari
Davis Mwamunyange katika viwanja vya Ikulu leo wakati alipopokelewa na
mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo.
Rais
wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan aki mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe
Magufuli leo wakati alipopokelewa kwenye viwanja vya ikulu jijini Dar es
salaam.
Msafara
wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan na mwenyeji wake Rais Dk.
John Pombe Magufuli leo wakipokea heshima kwa kupigiwa nyimbo za mataifa haya
mawili na mizinga.
Rais
wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akikagua gwaride katika viwanja vya
Ikulu leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli
leo.
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya
makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa
maendeleo baina ya nchi hizo.
Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu,
utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.
Akizungumza mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji
wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na
kimaendeleo baina nchini hizo.
Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep
Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi
huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa
ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza
uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba
mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande
cha ujenzi wa reli hiyo.
Rais magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika
la Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini
Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo
kukuza uchumi wa nchi hizo.
Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa
mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya
uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo,
Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.
Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo
baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye
malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya
Tanzania na Uturuki.
“Kiwango cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za
kimarekani 150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais
huyo.
Aidha Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia
nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.
Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa
makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii
yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu,
kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.
Prof. Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii
katika kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama
zilizopo nchini.
Wakuu
wa vikosi vya iulinzi na usalama wakisubiri kupokelewa kwa Rais wa Uturuki Mh.
Recept Tyyip Erdogan.
Makamu
wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa
wakati wa mapokezi hayo.
Baadhi
ya mawaziri na watendaji wa serikali ya Uturuki wakiwa wamekaa katika viwanja
vya Ikulu.
Waziri
wa Sheria na Katiba Dk. Harrison Mwakyembe kulia akiwa na Waziri wa Maliasili
na Utalii Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mapokezi ya Rais wa Uturuki Mh.
Recept Tayyip Erdogan.
No comments:
Post a Comment