Mkuu wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, akikagua masoko yaliyopomkoani humo ili kujiridhisha na hali ya chakula katikamkoa huo.
Na Mwamvua Mwinyi-Pwani
MKOA
wa Pwani, una ziada ya chakula zaidi ya tani 503,711.5 huku vyakula vikiwa
vimejaa kwenye masoko hivyo hakuna njaa.
Aidha
mkoa huo una mfumko wa bei za vyakula katika masoko mbalimbali kutokana na
kupanda kwa gharama za nafaka katika mikoa ya Mbeya,Kagera,Iringa na Morogoro.
Hayo
yalibainika ,katika ziara ya siku moja ya mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi
Evarist Ndikilo,alipotembelea soko la Mailmoja,Mlandizi na Chalinze kujionea
hali ya chakula.
Katika
masoko hayo mchele wa kawaida kwa sasa unauzwa kg kwa sh.1,500 hadi 2,000
,mchele super 2,200,unga sh,1600 ,mahindi 1,100 ,maharagwe kg sh.2,000 hadi
2,400 ,na viazi mbatata gunia sh.130,000 badala ya 60,000.
Mhandisi
Ndikilo alisema,msimu wa kilimo 2015/2016 mkoa ulilenga kulima
hekta 205,467 za mazao ya chakula zilizotarajiwa
kuzalisha tani1,039,565.
“Mkoa
pia ulilenga kulima hekta 158,242 za mazao mbalimbali ya biashara na
kutarajiwa kuzalisha tani 837,108 “alisema.
Mhandisi
Ndikilo,alisema hekta 144,241 za mazao ya chakula zililimwa na
kuzalisha tani 773,279 huku hekta 85,850 za mazao ya biashara zililimwa na
kuzalisha tani 566,283.
Alitoa
angalizo kuhusiana na upungufu wa utomwili (Protini) ambao hutokana na
uzalishaji mdogo wa mazao ya jamii ya mikunde.
Mkuu
huyo wa mkoa ,alisema upungufu wa mazao jamii ya mikunde, hauna athari kwani
hufidiwa na mazao yatokanayo na mifugo, uvuvi na mazao ya jamii hiyo kutoka
mikoa mingine.
Mhandisi
Ndikilo,alizielekeza halmashauri za wilaya
kuwajengea
uwezo wakulima kutambua umuhimu wa uvunaji bora, utunzaji wa chakula na kiasi
cha chakula kinachohitajika kaya kwa mwaka mzima.
Alisisitiza
endapo kutatokea janga la njaa kwa mkoa ,basi wakulima watumie fedha walizopata
kwenye mazao ya biashara kama korosho.
Alisema
wakulima wa zao la biashara la korosho katika msimu unaoisha walipata sh.bil.33
kwa tani 12,000 walizouza, hivyo watumie fedha hiyo kununua chakula ili kununua
chakula na kukabiliana hali hiyo.
Mhandisi
Ndikilo,alikemea kutumia nafaka kwenye shughuli zisizo za lazima,ngoma na
kutengeneza pombe .
Nae
afisa kilimo kutoka sekretarieti mkoani hapo,Judith Mushi,alisema hali ya
chakula kimkoa ni ya wastani lakini tatizo ni wananchi kulalamikia hali ngumu
ya maisha.
Alihimiza
kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukomaa haraka ikiwa ni sanjali na
muhogo, mtama, viazi vitamu na kunde.
Judith
aliwashauri wafugaji wauze sehemu ya mifugo yao ili kujinunulia chakula badala
ya kukaa na mifugo mingi bila tija.
Mfanyabiashara
wa nafaka katika soko la Chalinze, Saidi Ally, alisema wafanyabiashara
wanapandisha bei za vyakula kutokana na kununua bidhaa mbalimbali kutoka
mikoani kwa gharama kubwa.
Alisema
kwasasa pia wanagombania bidhaa hizo kwani zinashushwa magunia machache
kwasababu kilimo cha vuli na masika (hasa mazao ya chakula) haukuwa mzuri .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,akiangalia hali ya
chakula katika masoko mbalimbali Mailmoja,Chalinze na Mlandizi ili kujiridhisha
kuwa hakuna njaa mkoani hapo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
No comments:
Post a Comment