Jumuiya ya singasinga yakabidhi madawati 100 yenye thamani ya milioni 5, kwa shule ya Sekondari
Kiwangwa wilayani bagamoyo.
Wakizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo,
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete alisema anaishukuru jumuiya hiyo
kwa kuchangia madawati hayo kwani ni sehemu ya
kutatua changamoto mbalimbali katika shule hiyo.
alisema mambo ya maendeleo yanahitaji ushirikiano
baina ya wadau mbalimbaliili kufikia malengo ambapo jumuiya hiyo imekuwa miongoni
mwa wadau wanaojali maendeleo ya kijamii katika Halmashauri ya Kiwangwa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kiwangwa,
Malota Kwaga, alisema mahusiano mema baina jumuiya hiyo ya singasinga na
viongozi wa serikali ndiyo kilichowapa
moyo wa kuchangia.
Aliongeza kuwa viongozi wote kwa ujumla wan
athamini mchango wa wadau mbalimbali katika juhudi za kuisadia serikali kwenye
maendeleo ya kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, aliipongeza jumuiya hiyo kwa kutoa msaada
huo, na kwamba kama serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali
ili kuhakikisha maendeleo mbalimbali yanapatikana wilayani humo.
Alisema wilaya inakaribisha wawekezaji mbalimbali
kuwekeza na kuwataka kutoa ushirikiano waokatika shughuli za maendeleo ya
kijamii.
Aidha, aliwaomba wadau hao kusaidia swala maji
katika shule hiyo ambayo ina tatizo la upatikanaji wa maji.
Awali wakisoma risala kwa wageni waalikwa,
wanafunzi wa shule hiyo walisema shule
hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa jengo la utawala,
uhaba wa vyoo pamoja na maji.
Mara
baada ya zoezi la kukabidhi madawati hayo, limefanyika zoezi la upandaji miti
katika eneo la shule hilyo kwaajili vivuli ambapo viongozi wa singasinga, mkuu
wa wilaya, mbunge na Diwani wote walipata fursa ya kupanda miti.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete
katika hafla fupi ya kupokea Madawati kutoka jumuiya ya Singasinga shule
ya Sekondari Kiwangwa.
Katibu wa jumuiya ya Singasinga, Jasdeep, akizungumza wakati wa kukabidhi madawati 100, katika shule ya Dekondari Kiwangwa
Madawati 100 yaliyotolewa na jumuiya ya Singasinga katika shule ya Sekondari Kiwangwa
Mbunge wa Jimbo la Chalinze akipokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na jumuiya ya Singasinga katika shule ya Sekondari Kiwangwa
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,
akipanda mti katika shule ya Sekondari Kiwangwa
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga,
akipanda mti katika shule ya Sekondari Kiwangwa
Diwani wa kata ya Kiwangwa, Malota Kwaga,
akipanda mti katika shule ya Sekondari Kiwangwa
No comments:
Post a Comment