Monday, January 9, 2017

WANANCHI BAGAMOYO, WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA KILIMO CHA MPUNGA.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, akionyeshwa mashamba ya  Mpunga ya Chama cha Ushirika Tegemeo, na Mwenyekiti wa chama hicho,  Emanuel John .
 ..........................

Wananchi wa Halmashauri ya Bagamoyo, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua mashamba na  kulima,  katika mashamba ya  mpunga ya Chama cha Ushirika Tegemeo ili kuondokana na tatizo la njaa. 

Kauli  hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid   Mwanga,  alipokuwa akizindua  msimu wa kilimo  katika mashamba  ya  Mpunga ya chama cha Ushirika Tegemeo ambayo zamani yalikua  yakijulikana kama JICA.

Alisema Bagamoyo kuna  mito mikubwa ya  Ruvu na Wami ikitumika vizuriinaweza kuwaletea mazaoya kutosha  wananchi wa Bagamoyo  na kusaidia kuondoa tatizo  la njaa.

Akizungumzia swala la pembejeo, Mkuu huyo wa wilaya alisema tayari serikali imeshatoa  mbegu na mbolea  ambavyo vitapatikana kwa kupitia wakala atakaeteuliwa na serikali ya wilaya ili kukabiliana na changamoto ya gharama kubwa ya pembejeo.

Awali akisoma taarifa mbele ya mkuu wa wilaya, Mwenyekiti  wa Chama cha Ushirika Tegemeo, Emanueli  John, alisema  Chama hicho  kimepata mafanikio  kadhaa katika uzalishaji kutoka tani 2.5 hadi tani 4.5 kwa hekta.

Pamoja na mafanikio  hayo, Mwenyekiti  huyo wa Chama cha Ushirika Tegemeo,  amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili ni  pamoja na kukosekana kwa matrekta kwaajili  kulimia. 

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga ,  akiendesha Trekta la kulimia katika uzinduzi wa  msimu wa  kilimo  2017 katika mashamba ya Chama cha  Ushirika  Tegemo Bagamoyo.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, katikati, kushoto ni Mkurugenzi  wa Halmashauri ya   Bagam oyo,  Fatuma Omari Latu, kulia ni Mwenyekiti wa  Chama cha Ushirika Tegemeo, Emanuel John.


No comments:

Post a Comment