Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo amepokea mabati elfu
mbili yenye thamani ya shilingi milioni
40 kutoka kwa Kampuni ya Sayona Group ili kusaidia ujenzi
wa madarasa katika wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa wilayaya Bagamoyo, Majid Mwanga, alisema anaishukuru
Kampuni ya Sayona Group kwa kutoa
msaada huo ambao utasaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa
wilayani humo.
Alisema kwa sasa wilaya ya Bagamoyo imeweka
mikakati ya kuongeza vyumba vya madarasa kila kata ili kuondoa
uhaba wa vyumba vya madarasa
ambapo kwa sasa limekuwa changamoto kubwa.
Aliongeza kuwa mara baada ya
kukamilisha utengenezaji wa
madawati nguvu zote zim eelekezwa katika
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katika
mikakati hiyo ya ujenzi wa
madarasa wilayani Bagamoyo, Mkuu wa
wilaya hiyo, Majid Mwanga amekuja
na kauli
mbiu isemayo "UONGOZI UNAOACHA ALAMA" ambapo kwa kushirikiana na viongo wake mbalimbali Ngazi ya Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji wananchi
wamekuwa wakishiriki ilikufanikisha ujenzi huo.
Aidha,
alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuchangia ujenzi huo wa madarasa
wialyani humo ili kuleta dhana ya ushirikishwaji wa
maendeleo kati ya wan anchi na
serikali.
Kwa upande wake
Mkurugenzi msaidizi wa
Kampuni ya Sayona Group
,Aboubakari Mlawa alisema wamefikia uamuzi wa kutoa
msaada huo lengo likiwa ni k ui sai dia
serikali katika kuleta
maendeleo ambayo wan ufaika
wakubwa ni wananchi wenyewe.
Aliongeza
kwa kusema kuwa
Kampuni ya Sayona Group ambayo inajenga
kiwanda cha Juisi kataya Msoga wilayani Bagamoyo , ina wajibu wa kusaidia miradi m balimbali ya maendeleo kwakuwa kamapuni hiyo ni sehemu ya Bagamoyo.
Mkurugenzi
msaidizi wa Kampuni ya Sayona Group, Aboubakari Mlawa, akizungumza mara
baada ya kukabidhi mabati hayo.
No comments:
Post a Comment