MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA
MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA Na Allan Kitwe, Igunga MIRADI ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 Wilayani Igunga Mkoani Tabora imekaguliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda. Akiongea na wananchi katika maeneo mbalimbali ambako mwenge huo umepita Kiongozi huyo ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mabilioni ya fedha katika Wilaya hiyo. Amesisitiza kuwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa umeridhika na kazi iliyofanyika kwenye utekelezaji miradi ya wananchi ndio maana ameweka jiwe la msingi na kuzindua miradi yote kwa sababu imejengwa kwa ubora unaotakiwa. ‘Nakupongeza sana Mkuu wa Wilaya Sauda Mtondoo, Mkurugenzi Mtendaji Selwa Hamid na Wataalamu wote kwa kusimamia vizuri na kwa dhati fedha zilizoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hii’, ameeleza. Miradi iliyotembelewa na kuzinduliwa na Kiongozi huyo ni mrad...